Hatimaye Kampuni ya Simu ya Airtel yawatendea haki wana Gairo.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Airtel.

Kwa kiasi kikubwa
mtandao wa Airtel ndio mkombozi mkubwa wa wananchi wa Gairo hasa
vijijini. Bado mawasiliano ya simu ni changamoto kubwa sana Gairo.
Mhe. Mchembe
aliendelea kuwapongeza Airtel kwa ajira zaidi ya 400 nchini kupitia
ofisi zinazozinduliwa sasa. Vijana wa Gairo pia ni wafaidika wa Ofisi
hizo.
Kabla ya kufunguliwa
ofisi hizo, wananchi walikuwa wanaenda Dodoma au Morogoro kwa huduma
mbalimbali zinazohitaji kushughulikiwa na Airtel wenyewe.
Mhe. Mchembe
anayakaribisha mashirika mengine ya simu kufungua ofisi Gairo. Wilaya
inakuwa kwa kasi kubwa na mzunguko wa pesa ni mkubwa na mawasiliano
yanahitajika kwa kasi kubwa.
# Gairo Maendeleo Fasta kwa Mwendo Mdundo
# Hapakazitu
No comments:
Post a Comment