Pages

Wednesday, February 28, 2018

Wizara ya Mambo ya Nje Yaahidi Kutekeleza Diplomasia Ya Uchumi kwa Vitendo


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akitoa taarifa ya ufunguzi katika kikao cha Wizara na wadau kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Februari 2016.
Lengo la kikao hicho ni kujadili maandalizi ya maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayotarajia kufanyika Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 25 hadi 28 Aprili 2018 ambayo yanatarajiwa kwenda sambamba na sherehe za Siku ya Tanzania (Tanzania day) ambayo husherehekewa tarehe 26 Aprili 2018 siku ya Muungano. Maonesho hayo ni njia mojawapo za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi inayosisitiza katika kukuza biashara, utalii na uwekezaji.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akizungumza. Balozi Chana alieleza kuwa Ofisi za Ubalozi zimejidhatiti kuhakikisha zinasimamia fursa zote za Watanzania hususan masuala ya biashara ili kuweza kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.
Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi kuhusiana na maonyesho iliyokuwa ikiwasilishwa na Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Juma Ali Juma, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo  ya Biashara (TANTRADE), Bw.  Edwin Rutageruka.
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi Mtendaji-Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye na Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA), Bw. Godfrid Muganda.
Wajumbe kutoka Serikalini na sekta binafsi wakifuatilia kikao. Waliokaa mstari wa kwanza  ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe. 
Wajumbe wakifuatilia kikao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga na nyuma yake ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Bertha Makilagi.
Wajumbe wakifuatilia kikao.

Sehemu nyingine ya wajumbe wakifuatilia kikao.

No comments:

Post a Comment