Pages

Wednesday, February 28, 2018

WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) pamoja na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Mhe. Kim Nguyen Doanh (hawapo pichani)

…..Mkutano wa Waziri Mahiga na Balozi wa Japan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. Mazungumzo yao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya manufaa kwa nchi hizi mbili. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto)  Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw.
Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri.

No comments:

Post a Comment