Pages

Tuesday, January 2, 2018

Tigo Yapata Mamilionea Wapya wa Mwaka Mpya 2018


Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kulia) akiongea kwa njia ya simu na moja wa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde iliyofanyika usiku wa kuamkia mwaka mpya katika ofisi za Tigo ambapo Lugano Thomas Mlimi wa Dar es salaam, Kulthum Salim Ally wa Ruvuma na Maria Josef Maligisa wa Lindi walijinyakulia shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5 katika promosheni hiyo. Katikati ni Meneja wa Mapato wa Tigo, Arnold Ngakashi na kushooto ni Mwakilisi wa Bodi ya Michezo ya Bahati na Sibu Tanzania, Ally Abdallah.


Wateja watatu wajishindia TSH 15 milioni, 10 milioni na 5 milioni!
Wengine 150 wajinyakulia zawadi za TSH 1 milioni na 500,000 kila mmoja!
Dar es Salaam, 31 Desemba, 2017

‘Nimeanza mwaka mpya nikiwa milionea!’ alisema Lugano Thomas Mlini, ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam alipotaarifiwa kuwa amejishindia shilingi milioni 15 kutoka Tigo.  
Kupitia huduma yake ya Tigo Pesa, kampuni ya simu inayoongoza ya Tigo imewageuza Watanzania watatu kuwa matajiri wapya kwa mwaka 2018.  

‘Ndoto zangu za kuanzisha biashara sasa zimetimia! Ahsanteni sana Tigo’ alisema Kulthum Salim Ally, mkulima na mkaazi wa Tunduru, Ruvuma ambaye naye alijinyakulia kitita cha shilinigi 10 milioni katika drooo kabambe ya promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde iliyofanyika siku ya mkesha wa kuamkia mwaka mpya, katika ofisi ya makao makuu ya Tigo jijijni Dar es Salaam.
‘Nilienda kulala nikiwa maskini na sasa nimeamka nikiwa tajiri’ alisema Mariam Josef maligisa, Mkulima na mkaazi wa Nagangu, Lindi aliyeamka kutoka usingizini ili kupokea simu yake na kutaarifiwa kuwa naye amejishindia  TSH 5 milioni kutoka Tigo.

Akitangaza washindi katika droo hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema, ‘Tigo pesa ni zaidi ya huduma ya kufanya malipo. Ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo leo tumewawezesha wateja wetu kutumiza ndoto zao za msimu wa sikukuu na Mwaka Mpya kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Alibainisha kuwa Tigo imetoa jumla ya shilingi 120 milioni kwa watu 153 kutoka maeneo mbali mbali ya nchi. Wateja walishinda zawadi nono za kila siku baada ya kutumia huduma ya Tigo Pesa.

‘Pia tunajivunia mchango wetu katika kufanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Kupitia Tigo Pesa, tunawawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma na kupokea zaidi ya TSH 1.7 bilioni kila mwezi. Hii inawawezesha wateja wenyewe pamoja na jamii, huku ikichangia ukuaji wa uchumi wa nchi,’ aliongeza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Willima Mpinga alisema kuwa,’Tigo inawatakia Watanzania wote Mwaka Mpya wenye furaha na mafanikio. Tigo ni mtandao unaowaelewa zaidi wateja na kujibu mahitaji ya soko.  Tulizindua promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde kwa dhumuni kuu la kuwawezesha wateja wetu kushinda pesa zitakazowawezesha kutimiza malengo yao ya mwisho mwaka.’

Tigo Pesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu ya pili kwa ukubwa nchini.  Tigo Pesa ina mtandao mpana zaidi wa wakala na watoa huduma zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote.  Tigo Pesa pia ilikuwa ndio huduma ya kwanza Afrika Mashariki iliyowezesha wateja kutuma fedha kwenda nchi nyingine kwa kutumia viwango na fedha za nchi husika.

Tigo ndio kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ikijivunia huduma bora za sauti, SMS, intaneti yenye kasi ya juu zaidi ya 4G iliyosambaa katika miji 24 nchini, pamoja na huduma za kifedha. Mtandao wa Tigo pia ni maarufu kwa promosheni na ofa zake bunifu kwa wateja.

Tigo ilianza kutoa huduma zake Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu sasa ndio kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini ikiwa na wateja zaidi ya 11.6 milioni.

No comments:

Post a Comment