Pages

Thursday, December 28, 2017

MAMIA WAMZIKA MAREHEMU MAYAGE S MAYAGE


Na Said Mwishehe, Blogu  ya Jamii.
TASNIA ya habari imeombwa kuendeleza mapenzi baina yao kama walivyoonesha katika ugonjwa wa Mayage S. Mayage aliyefariki juzi.
Hayo yamesemwa leo  mchana huu na Padre John kaniki wa Kanisa Katoliki katika ibada ya mazishi ya marehemu Mayage iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es  Salaam.Padre Kaniki amesema maumivu aliyokua akipata kitandani Mayage wakati anaumwa aliyatoa kwa ajili ya watu anaowapenda ikiwemo wanahabari wenzie.
Alisema msiba ni sehemu ya kutubia kwa wale wanaobaki hivyo ni vema wote kuwa wanyenyekevu kwa Mungu.Amesema yeye binafsi alimfahamu Mayage  S. Mayage katika kipindi ambacho alikuwa anaunwa kwani alikuwa akimfanyia maombi na alichojifunza ni upendo na uvumilivu. 
"Alikuwa ni mtu mwenye upendo na huruma, ni vema tukaendeleza mema yake na kubwa zaidi ni kumuombea kwa  Mungu, "amesema Padre Kaniki. 
  
Mayage S. Mayage wakati wa uhai wake amesoma katika vyuo mbalimbali vya ndani  na  nje na baada ya kuhitimu amefanya kazi katika maeneo mbalimbali.
Ilipofika mwaka 1995 ndipo alipojiunga na kampuni ya magazeti ya Habari Coparation ambayo sasa ni New Habari na baadae alikwenda gazeti la Raia Tanzania. 
Akizungumza katika maziko ya Mayage S. Mayage, Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absaloum Kibanda amemuelezea Mayage kama mwandishi aliyeacha alama ya ujasiri na uthubutu katika taaluma. Kibanda amesema mchango wa Mayage katika tasnia ya habari na hasa uchambuzi wa habari za siasa."Mimi na Mayage pamoja na wengine tuliojaaliwa pamoja Habari Coparation, anayeweza kumzungumzia vizuri Mayage ni mhariri na mwalimu wetu kitaalum.
 Safari ya Mwisho ya aliyekuwa Mwandishi Mkongwe hapa nchini,Marehemu Mayage Steven Mayage imefanyika jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaamu 
 Wawakilishi kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu John Chacha na Ankal Issa Michuzi kwa pamoja wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiweka shada la Maua juu ya kaburi la marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
 Mmoja wa aliyefanya kazi na Marehemu Mayage,Ndugu Haji Dillunga akiweka shada la Maua juu ya kaburi la marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
 Sala ya Maziko ya Marehemu Mayage Steven Mayage ikiendelea katika Makaburi ya Mbweni Maputo,kabla ya kumlaza mpendwa wetu katika nyumba yake ya Milele,jioni
 
 Katibu NEC-Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwandishi mkongwe hapa nchini,Marehemu Mayage S. Mayage nyumbani kwake leo,Mbweni jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR.

No comments:

Post a Comment