Na Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali
imeyaagiza makampuni ya Bima hapa nchini kuhakikisha yanaajiri
watanzania badala ya sasa kuajiri wageni kutoka nje ya nchi ambapo ni
makampuni matano tu hapa nchini yanaendesha bima ya maisha kati ya
makampuni 31 yaliopo nchini huku mengi yakiwa ni kutoka nje ya nchi.
Akifungua
mkutano wa Taasisi za bima kutoka nchi 20 za bara la Afrika(African
Insuarence Organization) Naibu waziri wa Fedha Dkta Ashatu Kijaji
aliwaambia washiriki kuwa serikali ya Tanzania kwa sasa imejikita kwenye
...
uchumi wa viwanda na mchango wa sekta hiyo unahitajiki kufikia malengo
tarajiwa ya kukuza uchumi.
Ameagiza
sekta hiyo kuangalia upya muundo wa bima ya maisha ilikuweza kuendana
na sera za nchi hususani ya viwanda bila kusahau kilimo itakayosaidia
watanzania wengi kukuwa kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi ambapo pia
amewataka kufanyakazi zaidi kuongeza wigo wa ongezeko la wananchi
wanaojiunga na Bima ya maisha hapa nchini.
“Nimatarajio
yangu kuwa sekta ya bima hapa nchini itasaidia ukuaji wa kiuchimi kwa
wananchi kuweza kujiunga kwa wingi na hili natajia kwa siku mbili
mtakazokaa hapa mtajadili ni namna gani mtaweza kuisaidia serikali
kuweza kukuza uchumi hususani wa viwanda kwa malengo
mtakayojiwekea”alisema Dkta kijaji
Kwa
upande wake Kamishna wa Bima hapa nchini Baghayo Saqware amewambia kuwa
wananchi wengi wanahitajika kuanzisha uwakala wa bima ilikuwezesha
kukuwa kwa sekta hiyo ambayo wageni ndio wenye makampuni mengi kuliko
wazawa hivyo ni fursa adhimu kwani vigezo vya kuanzisha uwakala
vinalingana na sifa za watanzania wengi wa chini.
Akawataka
Watanzania kutumia nafasi hiyo kuweza kujiunga na bima ilikuweza
kujinufaisha kiuchumi kwani sekta hiyo itawasaidia kuweza kukopeshwa
fedha na mabenki bila kuhitaji kuweka bondi au dhamana ambazo wamekuwa
wakiwekeza kwa sasa kwenye taasisi hizo za kifedha.
Dkta
Saqware amesema kuwa sekta hiyo ni muhimili wa ukuaji wa uchumi ndio
maana wameweza kuchangia katika ukuaji wa kiuchumi na wao wamechukua
maagizo ya Naibu waziri wa Fedha kama changamoto ya kukuza sekta hiyo
hapa nchini.
Ambapo
amewataka wananchi kuanza kufikiria mitazamo yao kujiunga na bima ya
maisha ambayo kwao ni uwekezaji,kujikinga na madhara na mkombozi wa
familia zao pindi wanapopata maafa mbali mbali.
No comments:
Post a Comment