Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika
picha ya pamoja na watendaji wa TFDA wakati akizindua CHETI CHA MFUMO
WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO
9001-2015 tukio lililofanyika katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar
es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa
maelekezo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na
Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo wakatikati na Mwenyekiti wa Bodi ya TFDA
Dkt Ben Moses.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na watendaji
wa TFDA wakiwa wameshishika cheti cha mfumo wa Uhakiki Bora katika
Kiwango cha Kimataifa Cha Iso 9001-2015.
Meneja Uchunguzi wa Dawa na
Vipodozi Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo mbele ya Naibu Waziri Dkt.
Faustine Ndugulile wakati akitembelea maabara katika viunga vya Mamlaka
hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakwanza
kushoto akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu TFDA wapili, Mwenyekiti wa
Bodi ya TFDA Dkt. Ben Moses wa tatu, na wa mwisho ni Meneja uchunguzi wa
chakula Dkt. Mziray
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia
baadhi ya bidhaa zinazopelekwa TFDA kwa ajili ya Uchunguzi
…………………………………………………………………………………….
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Chakula , Dawa na
Vipodozi TFDA imetakiwa kuboresha udhibiti wa uingizaji wa Dawa,
Vipodozi na Chakula nchini kiholela ili kulinda afya ya Watanzania .
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile wakati wa kuzindua CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA
KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 leo jijini Dar es Salaam.
“Dawa ni kitu nyeti sana,
hatuwezi kuruhusu dawa feki kuingia nchini, mnafanya kazi nzuri sana
katika nyanja hii na muendelee na mpango huu ili kudhibiti uingizaji wa
vyakula visivyokidhi viwango na...
mahitaji ya watanzania, ” alisema Dkt.
Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa
TFDA wanatakiwa kuzingatia muongozo wa kupitisha vyakula na vipodozi
kwenye mipaka ya nchi kwa kuzingatia ubora na viwango vilivyoweka katika
kudhibiti uingizaji mbovu wa vyakula.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa TFDA Bw. Hiiti Silo amesema kuwa ili kuendelea kukidhi matakwa ya
wateja na mahitaji yao wameamua kuendana na kiwango cha kimataifa na
kuwaita ISO kuja kuhakiki ambapo wamefanikiwa kukidhi na kupata cheti.
“Shirika la Viwango la Kimataifa
ISO limehakiki ubora wa huduma zetu katika kukidhi mahitaji na matakwa
ya watumiaji wa huduma zetu na kutupatia cheti kinachoturuhusu kutoa
huduma nchini” alisema Bw. Silo.
Aidha Bw. Silo amesema kuwa wapo
bega kwa bega na Serikali ya awamu ya tano ianyoongozwa na Rais Dkt.
John pombe Magufuli katika kusogeza mbele gurudumu la afya hapa nchini
kupitia taasisi ya TFDA.
No comments:
Post a Comment