Pages

Thursday, November 2, 2017

MALI ZENYE THAMANI YA SH. BILIONI MOJA ZATAIFISHWA NA SERIKALI


6
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP Bw. Biswalo Mganga aliesimama akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma
16
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi wa pili kushoto akingalia nyaraka wakati taasisi zilizo chini ya wizara zilipokuwa zikiwasilisha
taarifa ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma
19
Baadhi wa Wabunge wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa za utekelezaji kutoka kwa watendaji wa serikali mjini Dodoma
…………….
Serikali imetaifisha mali zenye thamani ya Shilingi 1,200,000,000 kufuatia kushinda maombi sita (6) ya urejeshaji wa mali zilizotokana na ...
uhalifu nchini ambayo yaliendesha katika mahakama mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Bw. Biswalo Mganga alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma.
DPP Mganga alisema mali hizo zilitaifishwa kutoka katika mashauri mawili yaliyokamilika ni Injini aina ya Yamaha, jahazi (ark), pampu mbili (2) za maji, lita 15,885 za mafuta ya diesel, magari (5) aina ya Range Rover Sport EVoque na gari moja (1) aina ya Audi.
Amesema pamoja na kutaifishwa kwa mali hizo maamuzi mbalimbali yalitolewa kuhusiana na maombi hayo ikiwa ni pamoja na wahusika kutakiwa kutokufanya miamala yoyote ya kibenki kwa mashauri matatu (3) na shauri moja (1) linasubiri kusikilizwa.
Amesema Divisheni ya Mashtaka iliendelea kutekeleza jukumu lake la kuendesha mashauri ya jinai kwa kusimamia shughuli za utenganishaji wa uendeshaji wa mashtaka na upelelezi na uratibu wa kesi kubwa katika Mahakama mbalimbali chini.
Amesema jumla ya mashauri 180 ya jinai yalifunguliwa katika Mahakama ya Rufaa, kati ya mashauri hayo 129 yalihitimishwa na mengine 51 yanaendelea katika hatua mbalimbali na kuongeza kuwa kati ya mashauri ya jinai 6,678 yaliyofunguliwa, 4,006 yalihitimishwa na mengine 2,672 yanaendelea kusikilizwa.
Amesema mashauri yanayohusu wanyamapori yaliendeshwa katika mahakama mbalimbali nchini na katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2017 kulikuwa na mashauri 386, kati ya mashauri hayo 52 yalihitimishwa na watuhumiwa kupewa adhabu mbalimbali ikiwemo faini ya shilingi 228,035,080 na mashauri 334 yanaendelea kusikilizwa.
Amesema Divisheni ya Mashtaka ina mashauri 200 ya dawa ya kulevya ambayo thamani yake inazidi shilingi milioni 10 kwa kila shauri lililopo Mahakamani nchini huku mashauri 10 yalihitimishwa.

No comments:

Post a Comment