Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya mfuko wa NSSF Profesa Samweli Wangwe katika mkutano wa wadau wa NSSF AICC jijini Arusha
Na CHRISTIAN GAYA
Shirika la taifa la hifadhi ya
jamii (NSSF) ilianza 1964 kama idara ya serikali, mpaka kufikia mwaka 1975
mfuko wa taifa wa akiba ya wafanyakazi (NPF) ulipitishwa kuwa Shirika la Umma. Mwaka 1997 ulibadilishwa kutoka
Mfuko wa Akiba (NPF) na kuwa mfuko kamili wa hifadhi ya jamii (NSSF). NSSF huendeshwa kwa kuzingatia kanuni
za...
bima ya jamii na huratibiwa chini ya wizara ya kazi na ajira.
Dira ya NSSF ni kuongoza katika
utoaji huduma bora za mafao ya hifadhi ya jamii katika bara la Afrika ifikapo
mwaka 2020. Majukumu makuu ya NSSF ni uandikishaji, ukusanyaji wa michango, uwekezaji na ulipaji mafao
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini
ya mfuko wa NSSF Profesa Samweli Wangwe wakati wa mkutano wa saba wa wadau wa NSSF
kuanzia 18-20 Oktoba 2017 AICC Arusha anasema mpaka kufikia Juni 2016 mfuko uliweza kuandikisha waajiri wapya wapatao
2, 788, wakati kwa upande wa idadi ya waajiri mpaka kufikia juni 2016 ilifikia
kuwa na waajiri 25,328. Mpaka juni 2016
jumla ya wanachama wapya wapatao 107, 764 waliandikishwa na mpaka kufikia mwezi
Juni 2016 mfuko ulikuwa jumla ya
wanachama wapatao 1,087,227.
"Mpaka kufikia Juni 2016 mfuko uliweza kukusanya michango ya
wanachama ipatayo jumla ya milioni 724,079.00. Idadi ya wastaafu wanaopata
pensheni mpaka kufikia Juni 2016/17 walikuwa 12,704. Kima cha chini cha
pensheni kinachotolewa na NSSF ni Shs
100,000/- kwa mwezi wakati kima cha juu cha pensheni Shs 17,242,789/-. NSSF ni
shirika pekee Tanzania linalopandisha viwango vya pensheni kulingana na
mabadiliko ya kiuchumi na kwa mara ya mwisho pensheni iliongezwa Agosti 2016" anafafanua mwenyekiti.
Anasema kwa upande wa mabadiliko ya viwango vya pensheni ya NSSF, kufikia
Julai 1998 mpaka Juni 2000 kima cha chini cha pensheni kwa mwezi kilikuwa
shilingi 14,000/ mpaka sasa kima cha chini cha pensheni kimefikia shilingi
100,000/- kwa mwezi.
"Tathmini ya kitaalam ya
mwaka 2009 ya ILO, na zile zilizofanywa mwaka 2010 na 2013 chini ya SSRA
zinathibitisha ya kuwa NSSF ni shirika imara na lina uwezo wa kujiendesha na
kulipa mafao ya wanachama wake kwa miaka
6 bila kukusanya michango" profesa
anasema .
Profesa Wangwe anawahakikishia
wanachama na wadau ya kwamba huduma ya matibabu hutolewa bure, kufaidika na mafao ya matibabu hakuathiri
michango ya mwanachama kwa namna yoyote ile hata wakati wa kujitoa. Mafao
mengine yote ya muda mfupi kama kuumia kazini na uzazi hauathiri pensheni ya
mwanachama.
Anasema NSSF ni
shirika lililo imara na lina thamani ya Shs 3.0 trillion kwa hesabu za kuishia
Juni, 2016. Makadirio
ya thamani ya shirika kwa mwaka 2017 ni
Shs trillioni 4, NSSF ina
mtandao mpana wa ofisi 65 nchi nzima, Ofisi za Mikoa 27, Ofisi za Wilaya
zipatazo 12, na vituo vipatazo ofisi 26. NSSF ni shirika imara linaweza
kuendelea kulipa wanachama wake kwa muda wa miaka 6 bila makusanyo kwa mujibu
wa ripoti ya tathmini ya mfuko uliofanyika mwaka 2013.
Anataja baaadhi ya changamoto zikiwemo juu ya baadhi ya wanachama
kukimbilia kuchukua michango yao kabla ya kustaafu na mwisho wake huwa ni mateso na msongo wa mawazo, waajiri kutolipa michango ya wafanyakazi wao
kwa wakati, uelewa mdogo wa hifadhi ya jamii kwa watanzania na changamoto za uandikishaji
wa sekta isiyo rasmi wakiwemo wakulima na wavuvi.
Mwandishi wa makala hii ni
mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni, mshauri na mtaalamu wa masuala ya
pensheni. Kwa maelezo zaidi gayagmc@yahoo.com
unaweza kutembelea tovuti hakipensheni
monitor online na hakipensheni blog +255 655 13 13 41
No comments:
Post a Comment