Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mara
baada ya kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini
yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. (Picha na Lusungu Helela-
MNRT)
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Iringa Richard Kasesela wakiwa kwenye picha ya pamoja na Sekretarieti ya
Waandaji wa kongamano mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya
utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa
(Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha
Walimu cha Kleruu wakifuatilia maada inayowasilishwa kuhusiana na Mradi
wa SPANEST jinsi inavyoshirikisha wananchi katika masuala ya uhifadhi
mara baada ya kufunguliwa kwa... kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu
Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. (Picha na Lusungu
Helela- MNRT)
………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Eng. Ramo Makani, amefungua kongamano la maonesho ya utalii ya
Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa.
Kongamano hilo limefanyika kwa
muda wa siku moja katika Ukumbi wa Chuo cha Walimu wa Kleruu
likiwakutanisha wasomi na wahadhiri kutoka vyuo vikuu nchini, wanafunzi
pamoja na wadau wa utalii wanaofanya shughuli za kiutalii likiwa na
lengo la kutathmini na kuangalia namna mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
inavyoweza kunufaika kutokana na utajiri wa vivutio vya utalii
vilivyopo.
Sambamba na kongamano hilo,
maonesho hayo yanaendelea kufanyika hadi Oktoba 2 katika viwanja
katika viwanja vya Kichangani yakiwa yamewakutanisha Wajasiriamali
wadogo 350 kutoka kona zote za mikoa hiyo
Akizindua Kongamano hilo Naibu
Waziri Makani amewataka wananchi kuanza kuutupia macho utalii wa nje ya
hifadhi kwa kuwa watalii wengi kwa sasa hawaji kuangalii wanyamapori
pekee.
Amesema watalii wa siku hizi
wamechoka kuangalia wanyamapori wanataka kujifunza kuhusu utamaduni wetu
pamoja na vyakula vyetu vya kiasili.
Mbali na kuwa na utajiri wa
makabila tofauti tofauti, Makani alisema Nyanda za juu Kusini imejaliwa
kuwa na vivutio vya Malikale ambayo bado havijatangazwa vya kutosha.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii, Philip Chitaunga alisema Iringa inasifika kwa kuzalisha
wataalamu wa tasnia ya utalii kutokana na uwepo wa chuo Kikuu cha
Tumaini kuwa ndo chuo cha kwanza kutoa shahada ya Utalii lakini imekuwa
nyuma kiutalii akitolea mfano wa hoteli zinazojengwa ni za chini ya
kiwango licha ya watalaam kuwepo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, David Jamhuri alisema mkoa umejipanga
kuhakikisha kuwa fursa za utalii kwa mikoa ya Nyanda za juu Kusini
zinafunguka kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa wa kwanza kunufaika
kutokana namipango waliyojiwekea
Pia aliwataka viongozi wa
Kiserikali kila wanapopata nafasi ya kuzungumza na wananchi watumie
fursa hiyo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii
vilivyopo nchini.
Muongoza watalii wa Kampuni ya
Chabo Tours, Serafino Liduino aliitaka Serikali kuanza kuona umuhimu wa
kutoa mafunzo mashukeni ili kutengeneza kizazi kinachojua thamani ya
kuhifadhi mazingira ili vivutio asilia viendelee kuwepo kutokana na
tishio la mabadiliko ya tabia ya nchi yanajitokeza kwa sasa.
No comments:
Post a Comment