Pages

Sunday, October 1, 2017

ABIRIA 500 WALIOKUWA WAKISAFIRI NA NDEGE YA AIR FRANCE WANUSURIKA KIFO, INJINI MOJA YAZIMA, NDEGE YATUA KWA DHARURA




NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
ABIRIA 500 waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, kutoka Paris kwenda Los Angeles, Marekanmi, wamenusurika kifo baada ya moja ya inji za ndege hiyo kuharibika na kuzimika hivyo kuwadfanya mapailot kutua kwa dharura nchini Canada.
ndege hiyo aina ya Airbus A380 ililazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Goose Bay, Labrador, Mashariki mwa Canada Jumammosi Septemba 30, 2017 baada ya injini yake moja kuzimika.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, ndege hiyo iliyokuwa na mruko namba 66 iliyoruka kutoka uwanja wa Charles de Gaulle, jijini Paris, ilikuwa na abiria 500, na moja kati ya injini zake 4 ilipatwa na uharibifu mkubwa wakati ikipita juu ya bahari ya Atlantic, maafisa wa ndege hiyo walisema.
“Pailot waliofunzwa vizuri na wahudumu wa ndege waliobobea, walifanikiwa kudhibiti hali hiyo na hivyo kuiwezesha ndege kutua salama na hakuna abiria aliyejeruhiwa.” Maafisa wa shirika la ndege la Ufaransa walisema.

No comments:

Post a Comment