SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mjufti Abubakary Bin Zubeiry, amewaasa Waislamu nchini kuitunza amani kwani ni kama yai.
"Unajua yai lilivyo, ukilichezea
likakuponyoka na kudondoka chini, huwezi tena kulikusanya na kulitumia,
hivyo niwajibu wetu sisi Waislamu na wananchi kwa ujumla kuitunza amani
tuliyo nayo na huu ndio ujumbe wangu muhimu kwa leo hii." Alifafanua
Mufti Zubeiry baada ya ibada ya sala ya Eid Al Edh'ha na Baraza la Eid
lililofanyika Masjid (Msikiti) wa Taqwa, ulioko Ilala Bungoni jijini Dar
es Salaam leo asubuhi Septemba 1, 2017.
Mufti Zubeiry amesema, Mwenyezimungu
aliwaambia waliofarakana kuwa hawawezi kuingia peponi mpaka wakapatane
kwanza, na kwa hakika tunawaomba watu wote waliohitilafiana, wenye
chuki, wenye vinyongo, wenye vifundo, waondoshe na leo ndio siku ya
kukaa pamoja na kula pamoja, katika sikukuu hii ya Eid al hadh'ha,
alisema Mufti.
No comments:
Post a Comment