NA
K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
MAHAKAMA
Kuu nchini Kenya, imetengua ushindi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya
hasimu wake mkuu Raila Odinga, urudiwe ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1,
2017.
Mahakama
Kuu ya Kenya, imefikia uamuzi huo leo Septemba 1, 2017, kufiuatia maombi ya
Mgombea wa Muungano wa upinzani NASA, chini ya mgombea wake, Bw. Raila Odinga,
ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 8, 2017 na kumpa ushindi Rais Kenyatta.
Katika
maombi yake, Bw. Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo
na kuongezewa kwa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za
uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu
namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matoko.
Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.

No comments:
Post a Comment