………………………………………………………
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe jana tarehe 30 Septemba, 2017
amefungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayofanyika
kitaifa mkoani Iringa na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na
Serikali katika kupambana na Majangili kwa kutoa taarifa za siri
zitakazoweza kuwaibaini na kuchukuliwa hatua.
“Ili
kulinda uwepo wa rasilimali za utalii zilizopo kwa vizazi vya sasa na
vijavyo, ni lazima wananchi kushirikiana pamoja na Serikali katika
mapambano dhidi ya ujangili, mkiona mtu ananyemeleanyemelea huko porini
tuambieni tutamshukia kama mwewe, hizi rasilimali na zetu sote”
alisisitiza Prof. Maghembe.
Alisema
changamoto ya ujangili bado ipo katika baadhi ya maeneo hapa nchini,
alitaja maeneo hayo kuwa ni upande wa Pori la Rugwa na Selous karibu na
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo watu huingiza mifugo hifadhini kwa
kisingizio cha kutafuta malisho wakati huo huo wakifanya uhalifu wa kuua
tembo.
Prof.
Maghembe alifungua maadhimisho hayo pamoja na Maonesho ya Karibu Kusini
na maonesho ya wajasiariamali wa viwanda vidogo SIDO yaliyoshirikisha
wajasirimali kutoka mikoa ya nyanda zajuu kusini kwa lengo la kuonesha
bidhaa zao zitakazoweza kutumiwa na watalii pamoja na watoa huduma
hiyo.
Akifungua
maadhimisho hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Prof.
Maghembe alisema, kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kwa upande wa
Siku ya Utalii Duniani ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo
wakati ile ya Maonesho ya Karibu Kusini ikiwa ni “Utalii endelevu ni
nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
Alisema
sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa
kuchangia asilimia kubwa ya mapato ya Serikali, kuongeza ajira, kipato
cha jamii na kuchochea ukuaji wa sekta zingine.
“Utalii
ndio ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni
kwa asilimia 25, Aidha, inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na
asilimia 11 ya ajira zote nchini” alisema prof. Maghembe.
Alisema
mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani
milioni 1,353.29 mwaka 2011 hadi Dola za Kimarekani milioni 2,131.57
mwaka 2016.
Alisema
mchango huo umechagizwa na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi ambao
waliongezeka kutoka 867,994 mwaka 2011 na kufikia 1,284,279 mwaka 2016.
Hata
hivyo, alisema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi
za Serikali katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya
rasilimali, utangazaji, mazingira bora ya uwekezaji na ushirikiano
madhubuti baina ya sekta ya umma na binafsi.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani alisema
Serikali imekusudua kuhakikisha kuwa utalii wa nyanda za juu kusini
unakua juu zaidi uweze kutoa mchango stahiki kwenye pato la taifa.
Alitoa wito kwa wananchi kutunza vivutio vya utalii vilivyopo, kuhifadhi
mazingira na kupiga vita ujangili.
“Kwa
upande wa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla natoa witoe washirikiane
na Serikali kuweka mazingira bora na ya kuvutia katika maeneo yenye
vivutio vya utalii ikiwemo hoteli za kisasa kwa ajili kuvutia watalii
wa ndani na nje ya nchi kutembelea vivutia hivyo” alisema Mhandisi
Makani.
Nae,
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina masenza alisema katika kuunga mkono azma
ya Serikali ya kukuza na kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini
Serikali ya mkoa wake kwa kushirikiana na wadau wa utalii wameandaa
Mpango Makakati wa kukuza sekta hiyo mkoani humo. Mpango huo
umezinduliwa jana na Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe.
Kila
mwaka nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani huadhimisha Siku ya
Utalii tarehe 27 Septemba kwa lengo la kuhanasisha umuhimu wa sekta hiyo
katika kuleta maendeleo ya jamii, utamaduni, kukuza demokrasia, kutunza
na kuhifadhi mazingira, kujenga uchumi na kuimarisha mahusiano ya
kitaifa na kimataifa. Kilele cha Maadhimisho ni siku ya jumanne tarehe 2
Oktoba, 2017.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia),
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe, akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya
Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 2,
Oktoba. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani akizungumza katika maadhimisho hayo mkoani Iringa jana.
Mkuu wa Wilaya ya Iirnga, Richard Kasesela akiratibu shughuli nzima ya maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa
pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Utalii wa
Mkoa wa Iringa ambao umeandaliwa kwa lengo kuunga mkono azma ya Serikali wa kufungua
utalii wa Nyanda za Juu Kusini katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na
Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Amina
Masenza na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi
Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu
kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakionesha Mkakati wa Utalii na Jarida la Iringa baada ya uzinduzi rasmi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip
Chitaunga akiwa na baadhi ya washiriki wengine kwenye ufunguzi wa
maadhimisho hayo.
Baadhi ya Machifu wa Iringa waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatila ufungunguzi wake.
Sehemu
ya washiriki wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho
ya Karibu Kusini. Nyuma yao ni mabanda ya maonesho hayo.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), Naibu Waziri,
Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina
Masenza (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela
wakielekea kukagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Kichangani
Mkoani Iringa jana.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto)
akipimwa afya katika banda la MSD wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana.
KKauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa
Viwanda”.
akipimwa afya katika banda la MSD wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana.
KKauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa
Viwanda”.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa
pili kulia) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza moja ya bidhaa za wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wengine
pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia). Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

pili kushoto), akikagua kifaa maalum cha kuwashia umeme katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya
Iringa, Richard Kasesela (kushoto).

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Naibu
Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia kwake) wakipata maelezo katika
banda la Sido kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo wakati wa
maadhimisho ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini
yanayoendelea Mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu
kushoto), akikagua gari maalum kwa ajili ya mafunzo katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wanaoshuhudia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard
Kasesela (wa tatno kulia).

Naibu
Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Waziri wa Maliasili,
Prof. Jumanne Maghembe (kulia kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina
Masenza wakikagua vifaa vya mfumo wa umwagiliaji vilivyotengenezwa na
VETA katika maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa
pili kushoto), akisalimiana na Machifu wa Kabila la Wahehe katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana.
pili kushoto), akisalimiana na Machifu wa Kabila la Wahehe katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akionesha picha za nyayo za
Zamadamu wa Laetoli na Engaresero zilizogundulika Ngorongoro mkoani
Arusha takribani miaka milioni 3.6 iliyopita kufuatia tafiti mbalimbali
zilizofanyika kwa muda mrefu.
Katika
maadhimisho hayo kuna fursa za kuwaona wanyamaori mbalimbali ikiwemo
Simba kama wanavyoonekana kwenye banda lao maalum. (PICHA NA HAMZA TEMBA
– WMU)
No comments:
Post a Comment