Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na
Watoto Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na wazee kwenye Ukumbi wa Shule ya
Sekondari Dodoma wakati akifungua Kongamano la Wazee kuelekea Kilele cha Siku
ya Wazee Duniani Oktoba Mosi 2017.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi
akifafanua jambo kwa wazee walioshiriki Kongamano lililofanyika kwenye Ukumbi
wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee Tanzania Mzee
Sebastian Bulegi akitoa salamu za wazee kwa Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa
Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (hayupo Pichani)
wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wazee kuelekea Maadhimisho ya Siku ya
Wazee Duniani lililofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma .
Mtaalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Huduma
za Jamii Dkt. Daudi Kaale akijibu hoja mbalimbali za wazee kwenye Kongamano la
Wazee kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani lililofanyika Ukumbi
wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Baadhi ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara
wakifuatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Wazee kuelekea
Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani liliofanyika Ukumbi wa Shule ya
Sekondari Dodoma.
No comments:
Post a Comment