Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama wakibadilishana hati ya Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini humo. |
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati), Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (kulia) na Mwakilishi Mkuu Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama
(kushoto) wakielekea katika hafla ya kusaini mkataba wa msaada wa
Shilingi bilioni 1.4, kwa ajili ya Usanifu wa kina wa Barabara ya
Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan nchini Tanzania,
Mhe. Masaharu Yoshida (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) kabla ya kusainiwa
kwa mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 zilizotolewa na Japan kwa
ajili ya kufanya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi
Mwenge ili kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto), wakisaini
makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco
hadi Mwenge, yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa
Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara
hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida akibadilishana hati za makubaliano ya
utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge,
yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa Shilingi
bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo,
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru
Matsuyama (wa pili kushoto) wakisaini Mkataba wa makubaliano ya msaada
wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya Usanifu wa kina wa upanuzi
wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama
wakipeana mkono baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa makubaliano ya msaada
wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa
Barabara kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kushoto) na Balozi wa Japan
nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa tatu kulia) pamoja na maafisa
waandamizi kutoka Tanzania na Japan wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya hafla ya kusainiwa kwa Mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa
ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge,
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akibadilishana jambo na Mtendaji
Mkuu wa wakala wa Barabara Nchini-Mhandisi Patrick Mfugale, baada ya
Tanzania na Japan kutiliana saini makubaliano ya Japan kuipatia Serikali
msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa
upanuzi wa barabara ya kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia), akifurahia jambo katika
Mkutano na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa
pili kushoto) muda mfupi kabla ya hafla ya kusainiwa kwa mkataba wa
msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa Barabara
ya Morocco hadi Mwenge yenye urefu wa kilometa 4.3, Jijini Dar es
Salaam.(PICHA NA WFM)
|
TAARIFA
Dar es Salaam, Septemba 1, 2017:
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia
Tanzania ruzuku ya Yen milioni 69 sawa na Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili
ya kufanya usanifu wa kina wa awamu ya pili ya mradi wa upanuzi wa
barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es
Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa
saini Septemba 1, 2017, Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa niaba ya Serikali,
Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Satoru Matsuyama.
Tukio hilo limekwenda sambamba na
kuingia makubaliano kuhusu muda wa kukamilisha mradi huo pamoja na
kupeana taarifa ya namna mradi huo utakavyotekelezwa.
Mradi wa barabara hiyo yenye urefu
wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa
awamu ya nne ya barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka
(BRT phase IV).
Akizungumza baada ya kutiwa saini
wa makubaliano hayo, Dkt. Mpango amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika
itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya msongamano wa magari
kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Ameishukuru Japan kwa msaada huo
wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo katika awamu ya
kwanza, Japan ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 99.5. kujenga barabara
ya njia nne katika kipande cha kilometa 12.9 kutoka makutano ya barabara
ya Tegeta na makutano ya barabara ya Mwenge.
“Si mara ya kwanza kwa Japan
kuisaidia Tanzania, wanajenga barabara za juu katika makutano ya Tazara,
ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma hadi Babati
mkoani Manyara (km 188.15), Tunduru-Mangaka – Mtambaswala (km 202) na
barabara ya Iringa hadi Dodoma (259.9)” alisisitiza Dkt. Mpango.
Alisema kuwa upanuzi wa barabara
ya Bagamoyo si tu kwamba itapunguza msongamano wa magari Jijini Dar es
Salaam lakini pia utaunganisha Jiji na Bandari ya Bagamoyo ambayo ni
muhimu kwa ajili ya usafirishaji wa watu, bidhaa na huduma kutoka
Jijini, mikoa ya Pwani na maeneo mengine ya nchi.
Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu
Yoshida ameeleza kuwa kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa awamu ya pili ya
barabara ya Morocco hadi Mwenge kumekuja baada ya kukamilika kwa awamu
ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Tegeta hadi
Mwenge ili matokeo ya mradi huo yaweze kuonekana dhahiri.
Ameahidi kuwa baada ya kukamilika
kwa usanifu wa kina wa barabara hiyo, Serikali ya Japan kupitia JICA,
itasaini mkataba wa kuanza ujenzi huo Mwezi Juni mwakani.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama,
amesema Japan imeamua kufadhili mradi huo baada ya utafiti kuonesha kuwa
Barabara ya Bagamoyo ndiyo yenye msongamano mkubwa wa magari ambapo
inakadiriwa kuwa magari 52,000 yanapita kila siku katika barabara hiyo.
Alielezea matumaini yake kwamba
mradi huo utakapo kamilika utasaidi kukuza shughuli za kiuchumi katika
Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa ndicho kitovu cha biashara kwa maeneo
mengine ya ndani ya nchi na kimataifa na kuwaomba wataalamu pamoja na
TANROADS kuharakisha usanifu huo wa kina.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara Nchini-TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa ujenzi
wa barabara hiyo hautahusisha ubomoaji wowote wa makazi ya watu wala
majengo ya biashara.
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
No comments:
Post a Comment