Pages

Tuesday, August 1, 2017

WAZIRI DK. HARISSON MWAKYEMBE AIAGA TIMU YA TAIFA YA RAIDHA, WANARIADHA NANE WAENDA KUFUKUZA UPEPO KWENYE MBIO ZA LONDON

4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha walioagwa leo kwa ajili ya kwenda nchini Uingereza katika mashindano ya London Marathon yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa nane.
1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe akizungumza wakati alipokabidhi bendera ya taifa kwa wachezaji 8 wa Riadha walioagwa leo kwenda kwenye mashindano ya riadha ya London Marahon yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa nane nchini Uingereza, Hafla ya kuwaaga wachezaji hao imefanyika Hyatt Kilimanjaro Hotel  jijini Dar es salaam leo.
2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe akimkabidhi bendera ya taifa mwanariadha Alphonce Felix Simbu kwa niaba ya wenzake katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka.
3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe akishuhudia wakati Rais wa Chama cha Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akipongeza mwanariadha Alphonce Felix Simbu kwa niaba ya wenzake mara baada ya kukabidhiwa bendera ya taifa katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika leo jijini Dar es salaam  Hyatt Kilimanjaro Hotel , kutoka kulia Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari Bw. Yusuph Singu na  Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande.
5
Mwanariadha Alphonce Felix Simbu akizungumza wakati alipokuwa akiwashukuru Multchoice kwa kumpa ufadhili na kufadhili pia maandalizi ya kambi ya timu ya taifa ya riadha wakati wa hafla hiyo.
6
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akimshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harisson Mwakyembe, Multchoice pamoja na Jeshi la Wananchi kwa jinsi ambavyo wamejitoa na kusaidia timu ya taifa ya Riadha na kwamba kazi iliyobaki ni kuleta mafanikio katika mashindano yaliyo mbele yetu.
7
Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akizungumza katika hafla hiyo kama mdhamini wa timu hiyo kwa sasa ambapo amewaomba makampuni mengine kushiriki katika kuidhamini timu ya taifa ya Riadha ili kuleta mafanikio zaidi.
8
Kulia ni Meneja Mahusiano Multichoice Tanzania, Johnson Mshana na Shumbana Walwa Afisa Masoko Multchoice wakiwa katika hafla hiyo.
10
Meneja Mahusiano Multichoice Tanzania, Johnson Mshana akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.
11
Baadhi ya wanariadha wakitambulishwa katika hafla hiyo ya kuwaaga iliyofanyika leo Hyatt Kilimanjaro Hotel jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment