Mkurugenzi wa Shirika la
Watumishi Housing Company Dk. Fredy Msemwa akizungumza na waandishi wa
habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Golden Tower jijini
Dar es salaam wakati akitangazo mradi mpya wa Njedengwa mjini Dodoma
ambapo zinajengwa nyumba za awali 154 eneo hilo litajengwa zaidi ya
nyumba 500 , kulia ni Aisa Mawasiliano na Mauzo wa Shirika hilo Bi
Maryjane Makawia.
Mkurugenzi wa Shirika la
Watumishi Housing Company Dk. Fredy Msemwa akizungumza na waandishi wa
habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Golden Tower jijini
Dar es salaam wakati akitangazo mradi mpya wa Njedengwa mjini Dodoma
ambapo zinajengwa nyumba za awali 154 eneo hilo litajengwa zaidi ya
nyumba 500, Kutoka kulia ni Afisa Mauzo Irene Kasanda na Afisa
Mawasiliano na Mauzo wa Shirika hilo Maryjane Makawia.
Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mauzo akiwaelezea waandishi wa habari jinsi mradi
huo wa nyumba utakavyotekelezwa.
……………………………………………………………………………
Kampuni ya Watumishi Housing
Company, yenye dhamana ya uwekezaji katika nyumba na inayotekeleza
mpango wa taifa wa makazi kwa Watumishi, ina jukumu la kujenga nyumba
50,000 zitakazouzwa kwa mikopo nafuu ya muda mrefu kwa watumishi waishio
ndani na nje ya nchi. Mpaka sasa WHC imeishajenga nyumba maeneo
mbalimbali nchini ikiwa ni awamu ...
ya kwanza katika kutekeleza mpango wa
taifa wa makazi kwa watumishi na maeneo yaliyojengwa mpaka sasa ni
Morogoro Mkundi (50), Kisesa Mwanza (59), Magomeni Dar Es salaam (88),
Bunju B Mwabepande (64), Gezaulole Kigamboni (329) na sasa kuanza ujenzi
wa nyumba (159) katika makao makuu Dodoma .
Katika kuunga mkono uamuzi wa
serikali wa kuhamishia shughuli za serikali katika mkoa wa Dodoma kwa
nia ya kuboresha maendeleo ya nchi, Watumishi Housing tumejipanga
kuwajengea watumishi nyumba bora na za kisasa mkoani Dodoma katika eneo
la Njedengwa, lililopo mkabala na eneo la Kisasa Dodoma.
Kutokana na mpango wa serikali wa
kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma kuja na fursa nyingi ikiwa moja
wapo ni ya kuendeleza makazi ya watumishi ambapo kwa sisi WHC ni jukumu
la msingi sana kwetu kuhakikisha watumishi wanapata makazi bora na ya
kisasa kwa bei nafuu. Hivyo basi kutokana na fursa hii Watumishi Housing
imeandaa ardhi ya ekari 55 za ardhi katika mkoa wa Dodoma ambapo
tunategemea kujenga jumla ya nyumba 500. Nyumba 159 zitajengwa katika
awamu ya kwanza kwaajili ya watumishi
No comments:
Post a Comment