Akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya
elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la
majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na
kilimo Dk Joviter Katabaro kutoka Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar
es salaam pamoja na kuwekwa maeneo ya kuangaliwa kwanza ipo haja ya
kufanya zaidi ili kufikia malengo.
Dk Katabaro katika mada yake
alisema kwamba pamoja na serikali kutenga zaidi ya TZS
1.366,685,241,000.00 katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi huku
Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) ikipatiwa
sh 201,655,446,000/- kwa ajili ya elimu, alisema kwamba anaona ipo haja
ya kuongeza nguvu katika maeneo kadhaa ili kuweka sawa mazingira ya
kufundisha na kufundishwa.
Mkuu
wa Utawala na Maendeleo ya Uwezeshaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi
na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki
wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya
serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Katika mjadala huo wa kitaifa
uliodhaminiwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk
Katabaro alisema kwamba kwa sasa vifaa vya kufundishia na kujifunzia
vinakosekana katika shule nyingi na taasisi zinazohusiana na elimu na
hivyo kukwamisha ufanisi na tija katika elimu.
Aidha katika mada yake alitaka
juhudi inayofanywa ya kuweka sawa mizania ya walimu pale walipo wengi
kuhamishwa inabidi iendelee ili kuweka uwiano sawa wa elimu nchini.
Pia alisema kuwa uwiano wa sasa wa
walimu nchini sio sawa huku katika masomo, baadhi yakiwa na walimu wa
ziada na mengine yakiwa na upungufu mkubwa.
Profesa
wa Menejimenti ya Elimu kutoka Skuli ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Eustella Bhalalusesa (katikati) akifafanua jambo kabla ya
kumkaribisha muwasilisha mada (hayupo pichani) kuhusu bajeti ya elimu
baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano
ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo
lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwaka 2016 kwa mujibu wake
kulikuwa na walimu wa ziada katika masomo kadha huku kukiwa na upungufu
katika masomo mengine hasa Hesabu na Sayansi: Basic Mathematics – 7,291
(Upungufu);Biolojia – 5181 (Upungufu);Kemia – 5373 (Upungufu);Fizikia –
6873 (Upungufu);Kilimo 508 (Upungufu);Kingereza– 1267 (ziada); Jiografia
– 3281 (ziada); Historia – 4764 (ziada) na Kiswahili – 4795 (ziada).
Pamoja na masomo Dk. Katabaro
aliangalia bajeti hiyo katika maeneo muhimu yanayofanya mtoto kuwa na
akili kama viwanja vya michezo na upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya
kunywa na usafi.
Maji haya ni muhimu sana kwa watoto wa kike ambao usafi wao ndio siri ya mahudhurio ya shule kila siku.
Dk
Joviter Katabaro kutoka Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam
(UDSM) akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa
Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya
bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mada hiyo pia ilitahadharisha
kuhusu takwimu ikitaka zitumike vyema ili kuondoa mipango mibovu hasa ya
uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza na wale wanaoingia kidato
cha kwanza.
Wakati huo huo katika mada
iliyowakilishwa kwa pamoja kati ya Profesa haidari Amani na John
Shilinde, kilimo pamoja na kutegemewa na wengi na kuwa chachu ya
maendeleo ya viwanda bajeti yake iliyotengwa bado ni ndogo
Walisema kwamba sekta hiyo ilipata
kiasi cha karibu asilimia 10 ya bajeti nzima, bajeti ambayo ukiiangalia
utaona kwamba haiwezi kubadili kilimo.
Wamesema kwamba kilimo ambacho
huajiri asilimia 70 ya wananchi ikichangia asilimia 28 ya pato la taifa
huku ikipatia asilimia 30 ya mapato ya kigeni na kuchangia asilimia 65
ya mali ghafi, bado sekta haijapewa nguvu za kutosha kusonga mbele.
Makamu
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo, Peter
Lanya akizungumza machache kabla ya kumkaribisha muwasilishaji mada
(hayupo pichani) kuhusu bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni
kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya
serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wamesema kilimo kitabadilika kwa fedha za utafiti na sayansi na ubunifu ili kuiweka sekta katika hali bora zaidi.
Walisema kwamba sayansi na ubunifu ni kichocheo kikubwa cha mabadiliko katika kilimo.
Wataalamu hao walitaka bajeti
zaidi kwa ajili ya utafiti na maendeleo, kilimo cha umwagiliaji,
kuongeza ruzuku, kuboresha kilimo cha kisasa cha kutumia zana kupunguza
upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza kazi zenye staha vijijijni,
kuongeza mnyororo wa thamani na matumizi endelevu ya ardhi na maji.
Mtafiti
Mshiriki Mwandamizi kutoka ESRF, John Shilinde akiwasilisha mada kuhusu
bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku
moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika
elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam Mshiriki
William Mhoja akichangia mada kwenye kongamano la siku moja la
majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na
kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mtaalamu
wa masuala ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof Honest Prosper
Ngowi akishiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa
ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na
ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ni sehemu ya wadau wa kongamano la siku moja la
majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na
kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau walioshiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment