Mbunge
wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa na viongozi kutoka mfuko
wa pensheni wa PPF wakiwa katika Ardhi ya Hospitali ya halmashauri ya
Mji wa Mafinga wakati wa kukabidhi vifaa tiba vyenye dhamani ya shilingi
million sits.
Mbunge
wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa Sambamba n Mwenyekiti wa
halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga wakati wa kupokea msaada huu
mkubwa wa vifaa tiba kutoka PPF
Baadhi
ya madiwani na viongozi wa halmashauri ya Mafinga Mjini wakiwa kwenye
picha ya pamoja baada ya kupokea msaada wa vifaa Tiba vyenye thamani ya
shilingi million sita kutoka mfuko wa pensheni wa PPF
Na fredy Mgunda, Iringa
Mfuko
wa pensheni wa PPF umetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya
...shilingi milioni sita katika hospitali ya halmashauri ya mji wa mafinga
mkoani iringa.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo afisa mawasiliano kutoka PPF Lulu
Mengele alisema kuwa msadaa huo ni muendelezo wa kurudisha huduma kwa
wananchi kwa kile wanachochangia kwenye mfuko huo.
“Wananchi
ambao wamekuwa wadau wetu wakubwa wamekuwa wakichangia katika mfuko
wetu kitu kichosababisha turudishe fadhila kwa kuleta maendeleo ya moja
kwa moja kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo serikali imezidiwa na
ukiangalia maeneo ya afya ndio imekuwa changamoto kubwa kwa serikali
ndio maana tumeanzia huku ili kuisaidia serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais Dr John pombe Magufuli”alisema Mengele
Aidha
Mengele aliwataka wananchi kujiunga katika mfuko huo wa pensheni ambao
umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hasa kwenye huduma ya afya kwa kuwa
bima zao ni za bei nafuu lakini unatibu unachostahili kutokana na bima
yako hivyo naomba muendelee kujiunga kwenye mfuko wa PPF kwa usalama wa
maisha yenu.
“Ukitoa
elfu ishirini tu inakusaidia kupata hudumu nzuri za afya hivyo naomba
mjiunge na mfuko huu kwa kuwa ni msaada mkubwa sana kwenu hasa hapa
Mafinga ambako kunashughuli nyingi za kijamii ambazo ni hatarishi kwa
maisha yenu” alisema Mengele
Naye
katibu wa hospitali ya mafinga Bernard Makupa ameshukuru msaada huo wa
vifaa tiba kutoka PPF kwa kuwa vifaa hivyo vitakuwa Masada kwa
hospitali.
“Tulikuwa
na changamoto katika wodi za wazazi nilikuwa na upungufu mkubwa wa
vitanda pamoja na magodoro yake hivyo kupata msaada huu unatusaidia
kupunguza changamoto hivyo hivyo nawashukuru na kuwapongeza sana PPF kwa
kurudi na kutoa huduma kwa jamii husika”alisema Makupa.
Mbunge
wa jimbo la mafinga COSATO CHUMI amewashukuru PPF kwa msaada wa vifaa
tiba ambavyo vitaendelea kupunguza changamoto zilizopo katika hospitali
hivyo.
“Vifaa
hivi vya Tiba ni muhimu sana katika idara yetu ya afya kwa kuwa
inatupunguzia changamoto kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi na mikoa ya
Jirani wanayoitumia hospitali yetu ya Mafinga” alisema Chumi
Chumi
aliwataka wananchi wa Mafinga Mjini kujiunga na mfuko huo wa pensheni
kwa kuwa unamanufaa mengi sana hasa upande wa afya na ni muhimu kuwa na
bimaa ya afya ya PPF kwa kuwa hudama yao ni ya ukahika na salama.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga
aliwashukuru mfuko wa pensheni wa PPF na mbunge Cosato Chumi kwa msaada
huu mkubwa ambao kama halmashauri ingekuwa vigumu kutekeleza kutokana
halmashauri hiyo kuwa Mpya.
“Chumi
amekuwa mpambanaji mkubwa wa halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa kuleta
maendeleo katika idara mbalimbali hivyo tunakuomba uendelee kutusaidia
kutatua changamoto za halmashauri hii”alisema Makoga
No comments:
Post a Comment