Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa
Tigo, Wiliam Mpinga, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, kuhusu promosheni mpya ya Jaza Ujazwe ambapo simu za
kisasa 720 zitatolewa kila siku kwa washindi wa promosheni hiyo. Kulia
ni Mtaalamu wa Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Kaimu Meneja wa
Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akionesha moja ya simu aina ya
Teco S1 zitakazotolewa katika promosheni hiyo.
Mtaalamu wa Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma, akizungumzia promosheni hiyo.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni inayoongoza kwa maisha ya
kidijitali Tigo Tanzania, bado inawavutia wateja wake tena na prmosheni
kubwa ambayo itashuhudia wateja hao wakiondoka na simu za... mkononi za
kisasa (Smartphones) kila saa kwa saa 24 kila siku. Simu za mkononi
zitatolewa zikiwa na muda wa bure wa mawasiliano kwa mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za
kisasa (Smartphones) 720 zipo tayari kuchukuliwa katika kampeni ya
promosheni hii mpya. Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa
tu kwa kuzijaza simu zao muda wa maongezi kwa kukwangua kadi, e-pin au
TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo kwa ajili ya
kushinda moja ya Smartphones za Tecno S1 ambayo itakuwa tayari
kuchukuliwa kila saa, kila siku, katika siku saba za wiki.
Tofauti na promosheni nyingine ambapo ni
wateja wachache tu wanapata zawadi chache, promosheni hii ya Tigo
imethibitisha kusimama mahali ambapo kila mteja mmoja anazawadiwa kila
anapojaza. Washindi wa Smartphone ya Tecno S1 watafurahia mawasiliano
ya bure kwa mwaka mmoja ambapo zawadi nyingine za kushinda zinajumuisha
bonasi ya bure katika sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno ( SMS)
kulingana na muundo wa matumizi wa wateja.
Akitangaza zawadi hizo mpya, Kaimu
Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa kampuni
hiyo kwa mara nyingine tena imefurahishwa na mwitiko chanya wa wateja
kwa kampeni maarufu ya Jaza Ujazwe na ndiyo sababu imewafanya waongeze
zawadi za kuvutia zaidi pamoja na bonasi zaidi za kusisimua kama ishara
ya shukrani.
"Ni sehemu ya utamaduni wa Tigo katika
kutambua kuungwa mkono kusiko na ukomo ambao wateja wetu wametupa.
Ndiyo maana, tunaamini kwamba wanastahili kupewa shukrani kwa kujitoa
kwao kwa kwa ajili ya bidhaa na huduma zetu. Tuna furaha mara
nyingine tena, kuwapatia wateja wetu zawadi hizi, zitakazowawezesha
kuendelea kufurahia huduma zetu za maisha ya kidijitali ", alisema
Mpinga.
Tuzo za kusisimua zinaendana na
kuongezeka kwa miundombinu ya mtandao wa kisasa ya Tigo, aliongeza
Mpinga akibainisha kuwa kipaumbele muhimu cha kampuni kilikuwa
kikizingatia mahitaji ya wateja na kutoa suluhisho linalofaa
kushughulikia mahitaji hayo.
"Wateja wote wa Tigo wanastahili
kupokea tuzo; tunatarajia kukidhi mahitaji ya mteja ya kuwa na uzoefu
usio na dosari kila wakati wanapowasiliana kwa chapa zetu.
Tunaamini kuwa wateja wetu
watafurahishwa na zawadi hizi mpya ikiwa ni pamoja na bonasi kwa
dakika, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) au data wanazozawadiwa na hivyo
kuimarisha utamaduni wao wa mawasiliano, "alibainisha Mpinga.
No comments:
Post a Comment