Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewahamasisha
watumishi wa halmashauri ya wilaya Singida kufanyakazi kwa bidii pamoja
na kujenga upendo baina yao.
Jafo ametoa kauli hiyo leo asubuhi alipokuwa akipita akitokea katika ziara ya kikazi mkoani Mara.
Akiwa mkoani humo, Jafo amesimama kwa muda mfupi wilayani hapo ili awasalimie na kuwatia moyo katika utumishi wao.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida Rashidi
Mohamed Mandoa amemshukuru Naibu Waziri Jafo kwa upendo wake wa kusimama
wilayani hapo na kukutana na watumishi.
“Kitendo hichi kinawapa hamasa kubwa watumishi kwa kuona kwamba wanathaminiwa na viongozi wao,”amesema Mkurugenzi huyo
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
No comments:
Post a Comment