NA
PASCHAL DOTTO- MAELEZO
Serikali
imezitaka Taasisi za umma zinazotumia mkaa na kuni kubadilishiwa matumizi na
kutumia gesi katika shughuli zake ili kusaidia katika uhifadhi wa mazingira.
Hayo
yamesemwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Makamba amesema kumekuwa na jitihada mbalimbali katika kutatua tatizo la
matumizi ya nishati ya mkaa na kuni, ili kuweka mazingira safi kwa kutunza
misitu na kuepusha ukataji wa miti ovyo.
“Kama
mnavyofahamu asilimia 90 ya Watanzania wanatumia mkaa na kuni kama nishati ya
kupikia na mwanga, hii inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa sehemu za
vijijini ambapo shughuli ya utengenezaji wa nishati hii hufanyika”. alisema
Makamba.
Mnamo
mwaka 2016 Ofisi ya Makamu wa Rais iliandaa mkutano wa wadau kushauriana, kujadiliana
na kutoa mapendekezo juu ya hali hii ya ukataji miti ovyo, mkutano ambao
ulihudhuriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini, Chuo
Kikuu cha kilimo cha Sokoine pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali na zisiso
za Serikali katika kutafuta mbinu nishati mbadala kwa wananchi.
Katika
ripoti ya pili ya mazingira ya mwaka 2014 inaonesha kuwa Jiji la Dar es salaam
pekee linatumia wastani wa tani 500,000 ya nishati ya mkaa kila mwaka na
mahitaji haya yanaongezeka kila kukicha.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Taifa ya ufuatiliaji na tathimini ya Rasilimali za misitu
nchini, inaonyesha kiasi cha ekari milioni moja au hekta 372,000 zinaharibika kila
mwaka kiasi ambacho ni kiwango kikubwa
cha uharibifu wa misitu.
Aidha
Waziri Makamaba amefanya mikutano mbalimbali na wasambazaji wa gesi nchini na
kuwaasa kuwa chachu kwa taasisi za Serikali zinazotumia mkaa na kuni, kikubwa
ni kubadilisha kutoka kutumia mkaa na kuni na kufunga mitambo ya gesi.
Amezitaja
baadhi ya taasisi hizo ambazo mara
nyingi zinatumia kuni ili kupata nishati ya kupikia chakula kuwa ni pamoja na Shule
mbalimbali nchini, Magereza, Majeshi, Hospitali, na Vyuo mbalimbali.
Waziri
Makamba amesema Serikali imefanikiwa kuwashawishi wamiliki wa mitungi ya gesi
ya LPG na CNG na wamekubali kufunga mitambo ya gesi katika taasisi hizo ili kupunguza
matumizi ya mkaa na kuni.
Mwishoni
mwa mwaka huu (2017) Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuandaa na kuratibu
maonesho makubwa ya teknolojia ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuni
zinazotekelezwa na wadau mbalimbali nchini, pia kutakuwa na mashindano ya
ubunifu katika teknolojia hiyo muhimu kwa mazingira na misitu nchini.
No comments:
Post a Comment