Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Bima la Taifa (NIC), Samwel Kamanga akiweka saini katika kitabu chwa
wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho
ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Saba saba) yanayoendelea katika viwanja
vya JK Nyerere barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa
Habari wa Wizara ya Fedha na Mipango Josephine Majura.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akisaini
kitabu cha wageni katika banda la GEPF wakati alipotembelea banda hilo
katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Saba saba)
yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere barabara ya Kilwa, Jijini
Dar es salaam
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia) akipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa Bw. Elisante Maleko wakati
alipotembelea Taasisi hiyo iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na
Mipango katika banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa
ya Biashara (Saba saba) yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere
barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango Dorothy Mwanyika (kushoto) akipokea kitabu kutoka
Taasisi ya Uhasibu Arusha (T) (IAA) alipotembelea banda la Wizara ya
Fedha na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Saba
saba) yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere barabara ya Kilwa,
Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, Bw. William Erio (katikati) akizungumza na Jumanne
Nyamgunda Afisa Mwandamizi wa Bima wakati alipotembelea Shirika la Bima
la Taifa katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango lililopo katika
viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba saba) jijini Dar es
Salaam ambapo aliwapongeza kwa huduma nzuri, kushoto ni Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny
Mwaipaja na kulia ni Mwanaidi Shemweta Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
NIC.
No comments:
Post a Comment