Pages

Saturday, July 1, 2017

Mpina Awataka Viongozi Ilala Kuchukua Hatua Kali Kwa Wananchi Watakaokaidi Kutii Maagizo ya Serikali


2017-4-24-13-24-49_img-20170424-wa0005
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka viongozi wilaya ya Ilala kuwachukulia hatua kali watu wanaokaidi kutunza mazingira yanayowazunguka.   
Ameyasema  hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akishiriki katika zoezi la usafi wa kila mwisho wa mwezi.  
Amesema kuwa ili kuweza kuhakikisha zoezi hilo linatimia na kuwashirikisha wananchi wote,
ni lazima viongozi  wawachukulie hatua kali wananchi ambao wanakaidi kushiriki katika zoezi hilo kwa lipo kwaajili ya  kuiokoa jamii na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.  
“Ninyi viongozi mnatakiwa kuwachukulia hatua kali wale wananchi wachache wanaokaidi kushiriki katika usafi, kwani haiwezekani watu wailaumu Serikali kwa kila kitu, sisi viongozi wa juu tuleteeni wale walioshindikana ili tuweze kuwashughulikia,”amesema Luhaga.
Aidha, katika hatua nyingine, Luhaga amewataka wananchi kuunga mkono hatua za zinazochuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwani anania ya dhati kuleta maendeleo ya nchi. 
Hata hivyo, pamoja na hayo, Mpina ameongeza kuwa katika awamu hii ya TanoTanzania imepata Rais wa kipekee ambaye amekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kote

No comments:

Post a Comment