Na Mahmoud Ahmad Arusha
SHIRIKA la chakula Ulimwenguni, FAO, limeahidi kuendelea
kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wakulima wanazalisha
chakula cha kutosheleza na hivyo kuondoa tatizo la uhaba wa chakula kwa
baadhi ya maeneo hapa nchini.
Mwakilishi
wa FAO ,Fred Caferody,ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu kwenye
siku ya wakulima wa mazao mchanganyiko ya chakula na biashara kutoka
mikoa mbalimbali nchini yaliyofanyika kwenye viwanja wa taasisi ya
utafiti wa mazao, Seliani jijini Arusha.
Amesema
FAO, imekuwepo hapa nchini kwa miaka 40 imekuwa ikiandaa sera na
program mbalimbali za kilimo na chakula ili kuwezesha wakulima kuzalisha
chakula kinachotosheleza mahitaji kwa kushirikiana na serikali na swala
la kilimo na chakula ni sehemu ya jukumu lake kuhakikisha hakuna
upunfgufu wa chakula nchini.
Kwa
upande wake baraza la nafaka la Afrika mashariki, EAGC,limesema
litaendelea kushirikiana na vituo vya utafiti wa mazao ya kilimo kwa
nchi za afrika mashariki katika kutafuta masoko ya nje wakulima nchini.
Mkurugenzi wa fedha wa shirika hilo Drollah Ssebagala, amesema baraza la nafaka litakuwa likiwapatia wakulima taarifa za masoko kwenye nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia DRC congo, Malawi na Zambia Sudani na Ethiopia
Kwa
upande wake mkurugenzi mkuu wa utafiti wa mazao nchini kutoka wizara ya
Kilimo na Mifugo, Dakta Jackson Nkuba, amesema upo ugonjwa wa Manjano
unaoshambulia mahindi na hilo ni tatizo kubwa hivi sasa serikali kupitia wizara ya kilimo imeweka nguvu kubwa ili kuudhibiti ugonjwa huo.
Amesema kuwa ugonjwa huo ni tatizo kwa kuwa unashambulia mahindi yakiwa shambani na kunyauka hivyo mkulima anapata hasara .
Amesema
kuwa hayo ni maonyesho ya nne ya mnyororo wa mazao ya kilimo kufanyika
nchini ni maonyesho muhimu sana na yatapanuliwa katika kanda zingine
nchini lengo ni kuwezesha wakulima kupata teknolojia ya kilimo cha
biashara kutoka kilimo cha kujikimu .
Hivyo akayataka makampuni ya uzalishaji wa
mbegu bora kutoka kwenye taasisi za utafiti wa mbegu ambayo
yataongezeka ili kuwafikia wakulima ili kuwafikia wakulima waweze
kuzalisha mazao bora na kulima kilimo cha kibiashara.
Akifungua
maonyesho hayo Katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega,
amesema mpango wan chi katika kilimo ni kuendelea kushirikiana na baraza la Nafaka la nchi za afrika mashariki,shirika la kilimo na chakula ulimwengini, FAO na wadau wengine
Amewataka
watafiti wa mbegu kuhakikisha matokeo ya uutafiti wanazofanya
yanawafikia wakulima ili kuweza klkuleta tija vinginecvyo yasiopowafikia
walengwa hayawezi kuleta tija kwenuye kilimo.
Amezitaka
taasisi zingine binafsi kuongeza ushirikiano na serikali ili
kuharakisha maendeleo na upatikanaji wa mbegu bora za mazao aina
mbalimbali za mazao.
Amesema uzalishaji mdogo wa mazao unachangiwa na kilimo kisichozingatia utaalamu ,ukosefu wa masoko mazao kushambiliwa na magonjwa ucheleweshwaji wa pembe jeo kutokuwepo kwa vikundi vya wakulima miundo mbinu hafifu ya kuhifadhia mazao na kuendelea na kilimo cha kizamani.
Hivyo
akatoa wito kwa wataalamu wa kilimo kuanzisha mashamba darasa kila eneo
ili wakulima waweze kupata elimu na kubadilisha mbinu za kilimo kutoka
cha kujikimu na kuwa cha kibiashara.
Akawataka
viongozi wa vijiji kihakikisha kila kaya inatenga hekari moja
yitakayotokana na kilimo cgha mazao yanayotokana na mbegu bora
zilizofanyiwa utafiti na hivyo kuharakisha mabadiliko .
No comments:
Post a Comment