Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird,
wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo
wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza
maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa
matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird,
wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo
wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza
maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa
matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird,
wakibadilishana hati (mkataba) ya mkopo wenye riba nafuu wa Dola za
Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi
na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo),
jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw, Doto James akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) baada ya kutia saini makubaliano na Benki ya Dunia ya kuipatia
Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili
ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango
wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila (kulia) pamoja na baadhi ya
maafisa waandamizi wa Serikali wakishuhudia tukio la kutiwa saini kwa
mkataba wa mkopo wa riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 (shilingi
bilioni 180) uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kugharamia mpango
wa kuboresha elimu kupitia program ya lipa kwa matokeo (elimu bila
malipo), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella
Bird, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kusaini
makubaliano ya Benki yake ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa
Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu
ya msingi na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila
malipo), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella
Bird, akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)
baada ya kusaini makubaliano ya Benki yake ya kuipatia Tanzania mkopo
wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza
maboresho ya elimu ya msingi na
sekondari kupitia mpango wa lipa kwa
matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
……………………
Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania
mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya
kusaidia mpango wa Serikali wa miaka 11 wa Elimu bila malipo kuanzia
elimu ya msingi hadi sekondari nchini.
Kiasi hicho cha fedha ni nyongeza
ya Dola milioni 122 zilizotolewa na Benki hiyo katika awamu ya kwanza ya
utekelezaji wa maboresho ya elimu kupitia Mpango wa Tekeleza kwa
Matokeo Makubwa sasa-BRN, uliolenga kuondoa changamoto za elimu nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird
amesema wakati wa utiaji saini mkataba wa nyongeza ya fedha hizo kati
yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kuwa
nyongeza ya Dola milioni 80 imetokana na Benki hiyo kuridhishwa na namna
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dokt. John Pombe Magufuli,
ilivyosimamia kikamilifu mpango huo wa utoaji elimu bure na kuwanufaisha
wanafunzi wengi wakiwemo wanaotoka katika familia masikini.
Amesema kuwa uamuzi huo
umesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi,
kuongezeka kwa ufaulu, wanafunzi kujua maarifa ya hesabu, kusoma na
kuandika, utoaji wa ruzuku ya elimu kwa wakati, hatua ambayo pia
imesababisha kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa miundombinu ya shule,
changamoto ambazo anaamini zinapungua kupitia mkopo huo wenye masharti
nafuu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James ameishukuru Benki ya Dunia kwa kutoa fedha hizo
ambazo amesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa mipango ya Serikali ya
kuboresha elimu nchini na kuondoa changamoto zinazoukabili mpango huo
likiwemo ongezeko hilo kubwa la wanafunzi.
Bw. James ameeleza kuwa fedha hizo
zitasaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa, ubora wa eimu, ukaguzi wa
shule, upelekaji wa walimu, na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji
maalumu ili waweze kupata haki hiyo ya msingi ya elimu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila, amesema
kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa elimu wa lipa
kulingana na matokeo upitia mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za
Marekani milioni 122 zimetumika kujenga madarasa 1,400, matundu 3,390 ya
vyoo, mabweni 261, majengo ya utawala 9, mabwalo ya chakula 9 nyumba za
walimu 11, uchimaji wa visima vya maji katika shule nne na kukarabati
vyuo vya ualimu.
Amesema kuwa mkopo mpya wa dola
za Marekani milioni 80 uliotolewa na Benki ya Dunia hata kabla ya awamu
ya kwanza ya mradi huo kumalizika hapo mwakani, umeonesha nia ya dhati
ya Benki ya Dunia kusaidia maendeleo ya elimu nchini.
No comments:
Post a Comment