Pages

Sunday, July 2, 2017

ABInBev Yazindua Mafunzo ya Uongozi wa Kibiashara Kwa Wahitimu wa Vyuo Vikuu Nchini


unnamed
Wanafunzi UDSM wakisikiza kwa makini manufaa ya kujiunga na program ya Global Management Training ya ABInBev
1
meneja vipaji wa kampuni ya ABInBev Afrika ,Cindy Rautenrouch,akielezea mikakati ya kampuni hiyo kuandaa viongozi wa baadaye wa kuendesha shughuli za kampuni
2
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM)  Emmanuel Mwanuke akimuuliza swali Meneja Mikakati wa TBL Group,Magabe Maasa (kulia)wakati wa uzinduzi huo.
3
Baadhi ya wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakimsikiliza Meneja Mikakati wa TBL Group,Magabe Maasa ,(kulia) wakati wa uzinduzi wa program hiyo.
4
Meneja ukuzaji vipaji wa TBL Group,Lilian Makau ,na Meneja vipaji wa ABInBev Afrika , Cindy Rautenrouch (kulia) wakiwaonyesha wanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) jinsi ya kutuma maombi ya kozi ya mafunzo kwa njia ya mtandao wa internet
…………………..
Wasomi nchini hususani wahitimu wa vyuo vikuu wanaotarajia kumalizia masomo yao mwaka huu wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na mafunzo ya kimataifa ya uongozi wa kibiashara ambayo  yameanzishwa nchini na kampuni mama ya TBL Group ya ABIn Bev.
Akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mlimani wakati  wakati wa uzinduzi wa program ya mafunzo haya nchini,Meneja wa ukuzaji vipaji wa ABInBev kanda ya Afrika,Cindy Rautenrouch,amesema kuwa  mafunzo haya yameishaonyesha mafanikio makubwa katika nchi ambazo kampuni hiyo inaendesha  biashara zake na sasa  ndio yamezinduliwa rasmi  barani Afrika.
Alisema katika kipindi cha awamu ya kwanza ya mafunzo haya zimechaguliwa nchi za Afrika ya Kusini,Tanzania,Kenya na Nigeria na lengo kubwa ni kuwanoa vijana wahitimu wasio na uzoefu wa kazi kupata elimu na uzoefu na wakishahitimu kupatiwa fursa za uongozi wa vitengo mbalimbali katika biashara za kampuni zilizopo kwenye nchi mbalimbali.
“Ndoto yetu kubwa kama kampuni ni kuwaleta watu pamoja katika ulimwengu maridhawa (Better World) katika kutimiza ndoto hii na kuhakikisha bidhaa zetu zinaingia katika  masoko mapya moja  ya mkakati wake ni  kuvutia wateja wapya na kuondoa mipaka na ndio maana tunatoa fursa kwa wote kujiunga na kufanya kazi na sisi”.Alisema Rautenrouch.
Alisisitiza kuwa hii ni fursa pekee kwa wahitimu wa Kitanzania kutoka vyuo vikuu vyote. wanachopaswa kufanya ni kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao na wale watakaokidhi vigezo na kuchaguliwa wataungana na wenzao kutoka mataifa mbalimbali kupatiwa mafunzo kwenye program hii ijulikanayo kama Global Management Training Programme.
Rautenrouch alisema   kwa watakaofanikiwa  kujiunga watapata mafunzo kwa muda wa miezi 10 mfululizo ambapo wanapata mafunzo ya nadharia na vitendo ndani na nje ya kampuni kwenye nchi mbalimbali na kukutanishwa na kuzungumza na wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali za uendeshaji wa biashara na utawala.
“Wahitimu walengwa zaidi katika program hii ni waliohitimu katika fani za Biashara,Uchumi,Masoko,Uhasibu na fedha,Uhandisi na IT na fani nyinginezo wenye vipaji kwa kuwa kampuni yetu inaamini katika kuwekeza katika  viongozi wa baadaye na ndio maana tumekuja na mpango wa kuwaandaa”.Alisema.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliohudhuria semina ya uzinduzi,Paul Melkior  anayesoma shahada ya  kwanza ya baiashara alipongeza jitihada hizi na kuongeza kusema kuwa uwekezaji unaolenga kuleta manufaa kwa jamii ndio unaotakiwa kwa kuwa unafungua milango ya  ajira kwa watanzania na kuwapatia fursa za uongozi wazawa  baada ya kupatiwa mafunzo ya kitaalamu.

No comments:

Post a Comment