Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng.
Juma Kijavara (kulia), akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, eneo ambalo ujenzi wa gati ya pili
ya bandari hiyo utakapoanza kujengwa wakati Waziri huyo alipokagua vifaa
vya Mkandarasi vilivyowasili katika eneo la mradi hivi karibuni.
Baadhi ya Vifaa ambavyo vitatumika katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya Mtwara vikiwa vimeshawekwa site tayari kwa kuanza ujenzi. Ujenzi huo unakadiriwa kukamilika ndani y amiezi 22.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti ya Blue), akiangalia
vifaa vitakavyotumiwa na Kampuni ya M/S China Railways Construction
Engineering Group (CRCEG) na M/S China Railways Major Bridge Engineering
Group Co. ltd (CRMBEG) katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya
Mtwara, mkoani humo hivi karibuni.
………………………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameuagiza Uongozi wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kupeleka wahandisi wa kutosha katika
ujenzi wa Gati ya Mtwara ili kupata uzoefu katika kazi za ujenzi.
Akizungumza mara baada ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Bandari hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema
ushiriki wa wahandisi hao utasaidia kuwajengea uzoefu mkubwa na hivyo
kuokoa fedha nyingi ambazo zitatumika kwa kuwatumia wahandisi wa kigeni.
“Mradi huu unagharimu fedha
nyingi hivyo ni muhimu wahandisi wa TPA wakaja kujifunza kwa vitendo ili
mradi utakapokamilika wahandisi wetu watumike kufanya ukarabati na
matengenezo badala ya kusubiri kuwaleta tena wahandisi kutoka nje”,
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amesisitiza uongozi wa TPA
kutafuta wahandisi waliomaliza vyuo nchini ili waweze kujifunza kwa
vitendo kupitia mradi huo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo ili kupata
uzoefu.
Kwa upande wake, Meneja wa
bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara, amemhakikishia Waziri Prof.
Mbarawa kuwa tayari utekelezaji wa agizo la kutafuta wahandisi hao
umeshaanza na hatua inayofata ni kuwasili kwa wahandisi hao eneo la
madi.
Upanuzi wa bandari ya Mtwara
utahusisha awamu nne na awamu ya kwanza ambayo itagharimu kiasi cha Tsh.
bilioni 137 na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 22, kukamilika kwa
gati hiyo kutaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli ya ukubwa wa mita
300 na kukuza uchumi wa mkoa huo kupitia usafirishaji wa gesi, saruji,
korosho pamoja na makaa mawe.
No comments:
Post a Comment