Bi. Rose Mdami Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiiano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA akiwahudumia
wateja mbalimbali waliofika katika banda la Mamlaka hiyo ili kupata
huduma ya kupatiwa vitambulisho vya taifa katika maonyesho ya Biashara
ya Kimataifa yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wakitoa huduma kwa wananchi mbalimbali
waliofika katika banda hilo ili kupatiwa vitambulisho vya taifa leo.
Wananchi mbalimbali wakiwa
wamefurika kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa NIDA katika
maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakiendelea na kutoa huduma katika banda hilo.
No comments:
Post a Comment