Meneja wa Wakala wa Barabara
Nchini (TANROADS). Mkoa wa Lindi,Eng. Issack Mwanawima (mwenye koti la
draft), akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa (kushoto), hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maegesho
hayo, Mkoani humo, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi huo hivi
karibuni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akiangalia ujenzi wa wa
maegesho ya kivuko unaojengwa katika mkoa wa Lindi alipotembelea mradi
huo hivi karibuni. Mradi huo utahusisha maegesho ya kivuko na ujenzi wa
mita 150 za barabara ya lami upande wa Kitunda.
Tinga Tinga likiendelea na ujenzi
wa maegesho ya kivuko Mkoani lindi. Ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa
kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng.
Juma Kijavara (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), eneo la gati ya Lindi
ambalo litatakiwa kuchimbwa ili kuongeza kina cha gati hilo,
alipotembelea gati hiyo hivi karibuni.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng.
Juma Kijavara (katikati), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), wakati Waziri
huyo alipotembea alipotembelea gati la Lindi kuona hatua mbalimbali za
utekelezaji wa upanuzi wa gati hiyo hivi karibuni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akienda kuangali sehemu
ya kwanza ya upanuzi wa gati la Lindi ambalo kwa sasa linatakiwa
kuongezewa kina ili meli kubwa ziweze kutia nanga.
…………………..
Serikali imesema ujenzi wa
maegesho ya kivuko Mkoani Lindi utakamilika mwezi Novemba mwaka huu ili
kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa eneo la
Kitunda Mkoani Lindi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipokagua
maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo na kusema ujenzi huo umegharimu
kiasi cha Tsh, bilioni 1.8 ambazo zitahusisha maegesho ya Kivuko na
kujenga barabara ya kiwango cha lami mita 150 upande wa Kitunda Mkoani
Lindi.
‘Tuliahidi na sasa
tunatekeleza, nimefurahi kuona ujenzi unaendelea vizuri na
ninawahakikishia mwezi Novemba tutakuja kuzindua kivuko’ alisema WazirI
Profesa Mbarawa.
Aidha,Waziri Mbarawa amemtaka
Mkandarasi anaejenga magesho hayo kuzingatia thamani ya fedha wakati wa
ujenzi wake ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu.
‘hakikisha unajenga maegesho
haya kwa kuzingatia viwango tulivyokubaliana, hatutaki kuona kasoro mara
tu baada ya mwezi mmoja, hizi ni fedha za walipa kodi na tunategemea
miundombinu hii ikae muda mrefu’ alisisitiza Waziri Prof. MBARAWA.
Kwa upande wake Msimamizi wa
Mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), mkoa wa
Lindi, Eng. Issack Mwanawima amemuhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa
watasimamia mradi kwa kuzingatia viwango katika ujenzi huo na
kuhakikisha unakamilika kama mkataba unavyosema.
Katika hatua nyingine Waziri
Profesa Mbarawa amekagua maendeleo ya ujenzi wa Gati la Lindi na kusema
kuwa Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuongeza kina cha Gati hiyo
mara baada ya kutokea changamoto ya upana wa Gati hiyo kuwa mdogo.
‘Baada ya kujenga sehemu
iliyopo sasa tuligundua kuwa bandari inatakiwa kuongezwa kina hivyo
tukalazimika kufanya usanifu upya ili tuongeze upana wa mita 60 mpaka
500kwa eneo lote vinginevyo meli zisingeweza kufunga nanga’ alisisita
Waziri Prof Mbarawa.
Waziri Prof. MBARAWA aliongeza
kuwa lengo la Serikali katika kufanya usanifu upya ni kuhakikisha Gati
ya Lindi inakidhi mahitaji halisi na kuchochea uchumi wa mkoa huo.
Kwa upande Meneja Bandari ya
Mtwara Eng. JUMA Kijavara amesema Mamlaka ya Bandari Nchini TPA
imejipanga na iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na Mkanadarasi
ili aanze kazi hiyo.
Mradi wa upanuzi wa Gati la Lindi utahusisha miradi ya Gati hiyo, Bandari ya Lushungi pamoja na bandari ya Kilwa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment