Moovn Driver Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni hiyo,Godwin Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kwenye
ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akizungumzia kampuni yake
ya Moovn Driver kuhusu huduma ya usafiri kutumia Aplikesheni
waliyoibuni.
Moovn Driver Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni hiyo,Godwin Ndugulile akionysha jinsi aplikesheni ya Moovn
Driver inavyofanya kazi mbele ya waandishi wa habari.
……………………………………………………………………..
TANZANIA inatarajia kunufaika na
teknolojia ya kisasa ya usafirishaji ya Moovn Driver, kwa watu
wanaohitaji kupiga simu ya mkononi kuhitaji usafiri.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni hiyo,Godwin
Ndugulile amesema huduma hiyo itawasaidia madereva wa taksi, pikipiki
na bajaji nchi kufanya biashara kwa wakati na kukuza kipato chao na nchi
kwa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kufanya huduma hiyo kuwa ya uaslama
zaidi.
Amesema mtu atahitaji usafiri wa
taxi au bodaboda, bajaji kwa nyakati tofauti ataweza kupata huduma hiyo
kupitia teknolojia tuliyoibuni kupitia vijana mainjinia wa masuala ya
Teknohama ambao ni watanzani wa hapa hapa nyumbani Tanzania na kupelekwa
popote aendapo.
Ndugulile amesema kuwa dereva huyo kwa mfumo huo ataonekana kila sehemu atakapokwenda kupitia tekinolojia hii.
Amesema watumiaji satelaiti
ambapo abiria atakapo kuwa akiitumia kumtafuta dereva itamuonesha dereva
aliyekuwa karibu yake na kuongeza kuwa endapo dereva huyo naye atakuwa
akiitumia atapata taarifa kuwa katika eneo Fulani kuna abiria.
Alisema aplikesheni hiyo
inapatikana bure kwa wateja wote ili kuweza kutoa huduma nafuu kwa
vyombo vya usafirishaji mbalimbali kama taxi bodaboda, na bajaji.
Amesema madereva wataongeza
kipato, watarahiaisha biashara, usalama dhidi ya mteja aliyempakia,
mawasiliano, ripoti ya mapato na malipo ya kirahisi ya kulipwa kwa njia
ya mtandao kupitia teknolojia hiyo.
Wakati kampuni nyingine
zinamkata dereva asilimia 25 mpaka 45 ya mapato ya siku na haziruhusu
kupokea Bakshishi kutoka kwa mteja kampuni hiyo ya Moovn Driver
itamkata dereva asilimia 15 tu ya mapato yote ya siku ikiwa ni pamoja na
kumruhusu dereva kupokea tipu au (Bakshishi) kutoka kwa mteja.
Kabla ya kuanza kwa huduma hiyo
serikali imeshirikishwa ambapo pia Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
Kamanda Mohamed Mpinga alitaarifiwa kuhusu huduma hiyo ambayo italeta
tija na manufaa kwa kupunguza uhalifu, uwezo wa kukusanya kodi sahihi ya
mapato ya madereva na kuongeza kipato,ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
madereva wanafuata sheria na vibali na kurahisisha ajira.
Ameongeza kwa kuwahamasisha
madereva kujiunga na huduma hiyo ambayo itakuwa na faida kubwa kwao
lakini pia itawafanya kuendesha kazi zao kwa usalama zaidi kwa kuwa
watakuwa kwenye mfumo wa Setilaiti hivyo kuimarisha pia usalama wa
wateja.
No comments:
Post a Comment