Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikagua nyumba
iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na
afisa mtendaji wa kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti Juni 29,
2017 alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji hayo.(PICHA NA HASSAN MNDEME WA JESHI LA
POLISI)
IGP Sirro akisalimiana na wananchi wa
kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole
baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji.
Mkuu wa Meshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti mkoani Pwani Juni 29, 2017
alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na
afisa mtendaji wa kijiji hicho. IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi
kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo na kuwataka
kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.
No comments:
Post a Comment