Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda Baada ya
kuwasili mkoani humo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi
akizindua mpango kabambe mkoani Mtwara na Mkukabidhi Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara Bi. Halima Dendego.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua
mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi katika Halmashauri ya
Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanafanyika kwa ukamilifu.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua
masijala ya ardhi halmashauri ya Manispaa ya Mtwara na kuwataka Maafisa
Ardhi kuweka kumbukumbu za Hati Miliki za Ardhi katika mpangilio mzuri
ili kuepusha migogoro ya ardhi..
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiongea
na wananchi wa mkoa wa Mtwara katika uzinduzi wa Mpango Kabambe Mkoani
hapo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wapili
kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego (wakwanza kushoto),
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda (wakwanza kulia), Mwenyekiti
wa CCM Mtwara Ndugu Muhamed Sinani (wapili kulia) wakiwa katika uznduzi
huo.
Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakifuatilia Uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mtwara.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
……………………………………
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya uzinduzi wa Mpango
Kabambe (Master Plan) ya 2015-2035 Mkoani Mtwara . Katika shughuli hiyo
Mh. Lukuvi aliwataka watendaji wa Mtwara katika sekta ya ardhi kwa kwa
kushirikiana na ofisi ya
mkuu wa mkoa Bi. Halima Dendego kuhakikisha
kuwa wanafuata Master Plan hiyo ili kuweza kuipanga Mtwara na kanda ya
kusini yote vizuri hatimaye kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati na
Viwanda.
Katika ziara hiyo, mbali na
kuzindua mpango kabambe pia alifanya ukaguzi katika mifumo ya ukusanyaji
wa kodi ofisi za ardhi za halmashauri ya manispaa ya Mtwara ili
kuhakikisha makusanyo ya kodi ya ardhi yanafanyika kwa malengo mahususi.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi.
Halima Dendego akiongea na wananchi mbele ya Waziri Lukuvi,
alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa atasimamia utekelezaji wa mpango
kabambe kikamilifu kwa maendeleo ya watu wa Mtwara na watanzania kwa
ujumla.
Katika uzinduzi huo Mkurugenzi
Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje ameeleza kuwa
uzinduzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au koundoa kabisa
tatizo la migogora ya ardhi mkoani mtwara, na kuchochoea fursa za
uwekezaji, hivyo amewapa rai wananchi wa Mtwara kufuata mpango huo kwa
maendeleo ya taifa.
Pia Ndugu Hamza Sikamkono Afisa
Mipango Miji Manispaa ya Mtwara ameeleza kuwa dira ya mpango kabambe huo
ni kuwa na mji mahiri wenye uchumi wa mafanikio ambao hutoa kazi na
fursa za kutosha na kuvutia uwekezaji.
Afisa huyo ameeleza mpango huo
umegusa maeneo ya Naumbu, Mjimwema, Nanguruwe na Ziwani ukigusa huduma
zote za kijamii ikiwemo shule na hospitali na shughuli za kiuchumi
yakiwemo maeneo ya viwanda na uwekezaji.
No comments:
Post a Comment