Mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi
na Gylfi Sigurdsson umeipatia Swansea pointi muhimu ikihaha kubakia
katika Ligi Kuu ya Uingereza na kuharibu hesabu za Manchester United
kutinga katika nafasi ya nne.
Sigurdsson alipiga shuti la
kuzungusha kutoka umbali wa yadi 30 lililotinga wavuni huku kipa
akibaki anauangalia mpira, na kufanya matokeo kuwa 1-1 baada ya awali
Wayne Rooney kufungwa kwa mkwaju wa penati.
Kwa matokeo hayo Manchester United
imebakia katika nafasi ya tano, pointi moja nyuma ya mahasimu wao
Manchester City ambao wanapointi 66 sawa na Liverpool iliyokatika
nafasi ya tatu zikiwa zimecheza michezo sawa.
Wayne Rooney akifunga kiufundi mpira wa penati kwa kumpoteza mahesabu kipa
Mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na Gylfi Sigurdsson ukielekea kutinga wavuni
TOTTENHAM HAIJAKATA TAMAA YAENDELEA KUIFUKUZIA CHELSEA
Tottenham imejihakikishia kuwa
inaendelea kuwa nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea kwa
tofauti ya pointi nne baada ya kuwafunga wapinzani wao Arsenal kwa
magoli 2-0 katika dimba la White Hart Lane.
Ushindi wa Chelsea 3-0 dhidi ya
Everton uliipa presha Tottenhma lakini walijibu mapigo kwa staili nao
kwa kupata ushindi na kuendelea na kiwango bora, ikilinganishwa na
cha Octoba 1960 waliposhinda michezo 13 mfululizo.
Mchezo wao huo dhidi ya Arsenal
uliamuliwa na magoli yaliyofungwa na Dele Alli katika dakika ya 55
likiwa ni goli lake la 21 katika msimu huu, na kisha baadaye Harry
Kane akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penati.
Mchezaji nyota kijana Dele Alli akifunga goli la kwanza la Tottenham
Harry Kane akijipinda na kuachia shuti la mkwaju wa penati aliopiga kiufundi na kufunga goli la pili
CHELSEA IMEDHAMIRIA KUTWAA UBINDWA LIGI KUU YA UINGEREZA
Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza
Chelsea wamepiga hatua kubwa katika kuelekea kutwaa ubingwa baada ya
kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Everton katika dimba la
Goodison Park.
Chelsea ilipata goli la kwanza kwa
shuti kali la Pedro la umbali wa yadi 25, kisha Gary Cahill alifunga
la pili kwa shuti la karibu kabla ya Willian kufunga la tatu na
kuifanya iendelee kuongoza kwa tofauti ya pointi nne.
Kwa ushindi huo Chelsea hata
wakipoteza pointi tatu katika michezo minne iliyosalia bado wataweza
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, hata kama Tottenham
watashinda michezo yote iliyosalia.
Pendro akiachia shuti kali lililozaa goli la kwanza la Chelsea
Gary Cahill akiifungia Chelsea goli la pili katika mchezo huo
No comments:
Post a Comment