Pages

Thursday, March 2, 2017

MPINA ABAINI MADUDU MRADI WA MABADILIKO YA TABIANCHI


1
Naibu Waziri Mpina (katikati) akiwa na ujumbe wake, akisisita jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika Delta ya Rufiji kaskazini.
2
Naibu Waziri Mpina  (kaikati) na Ujumbe wake katika picha wakitembea kukagua mikoko iliyopandwa katika Delta ya Kaskazini Rufiji.
3
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake wakiwa katika Boat, wakielekea katika ukaguzi wa upandaji na utunzaji wa Mikoko, pamoja na uharibifu wa Mazingira katika Delta ya Rufiji Kaskazini.
4
Naibu Waziri Mpina akiwaasa wasimamizi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika delta ya kaskazini Rufiji hawapo pichani wamueleze ukweli kuhusu matumizi ya fedha na hali halisiya mradi kabla ya kwenda kukagua upandaji, utunzaji wa mikoko na uharibifu wa mazingira.
…………………………………
NA – EVELYN MKOKOI -RUFIJI
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina
amebaini madudu katika matumizi ya sh. milioni 396 za ufadhili wa Mfuko wa
nchi maskini zaidi duniani (LDCF) chini ya mkataba wa dunia mabadiliko ya tabia

nchi katika utekelezaji wa mradi wa upandaji na uendelezaji wa mikoko
katika delta ya kaskazi mto Rufiji.
Katika mradi huo matumizi ya zaidi ya sh. milioni 364  mchanganuo wake
hauridhishi huku vikundi vinavyodaiwa kulipwa fedha hizo vikikana kulipwa
na kusema hawakuwa na mkataba bali walifanya kazi kama vibarua kwa posho ya
sh. 10000 kila wanapomaliza kazi na hawakuwa na mkataba.
Kutokana na hatua hiyo Mpina amemuagiza Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Makamu wa Rais, Mwatano Maganga kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anafanya uhakiki wa matumizi ya fedha hizo za mradi na kuelekeza hatua za kuchukua kwakuwa
vielelezo alivyokabidhiwa na Msimamizi wa mradi kutoka Halmashauri ya
Rufiji Sabastian Gaganijas vina mashaka. “Naagiza ukaguzi ufanyike, lazima kuna ubadhilifu umefanyika katika utekelezaji wa mradi, baada ya ukaguzi makini, tutajua ukweli na kubaini hatua gani zitachukuliwa.” Alisisitiza Mpina.
Hata hivyo, baada ya zoezi zima la kukagua Delta hiyo yenye kilomota zaidi ya
15 Naibu Waziri Mpina, alisema amesikitishwa na jutekelezaji wa  mradi huo unaotumia  fedha za wafadhili zaidi ya sh.milioni 396 kuwa na madudu na amejionea mwenyewe  kuwa, mradi hauna usimamizi na kusema kuwa,  kuna
dalili ya fedha hizo kutumika ndivyo sivyo kwakuwa hata hekta 792 kati ya
1000 zilizodaiwa zimepandwa ni udanganyifu wa wazi.
“Huu ni uhuni ambao haukubali kwa serikali hii awamu ya tano tuliposema
hapa kazi tu tulimaanisha kuwa hatuwezi kudanganywa watu wamezoea kuona
Waziri hawezi kuja kwenye mazingira kama haya nimejionea mwenyewe mikoko
iliyopandwa haendani na thamani ya matumizi ya fedha hizo na sehemu kubwa
imevamiwa na kupandwa mpunga badala ya mikoko,”alisema.
Alisema katika mchanganuo aliokabidhi na msimamizo wa mradi fedha hizo
zaidi ya  sh.milioni  364 zimedaiwa matumizi yake ni pamoja na kulipa
vikundi 28 vilivyokabidhiwa mradi ambavyo sasa havipo.
Alisema cha kushangaza katika fedha hizo kipo kikundi kimelipwa zaidi ya
milioni 30 kwa kupanda hekta 3 huku kingine kikilipwa milioni 3 kwa hekta
hizo hizo.
Baadhi ya wakazi wa rufiji wakizungumza katika ziara ya Naibu Waziri Mpina, wametoa changamoto zao katika kukabiliana na uharibifu huo wa Mazingira   na kuiomba Serikali kuongeza usimamizi madhubuti katika mradi huo ili kukubaliana na uharibifu huo wa hifadhi hiyo ya mikoko,
Awali Imeelezwa na mtaalam wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu  wa Rais Bw. Cretus Shengena kuwa, uharibifu huo waMikoko unaweza kusababisha kupotea kwa uoto asili na baiyonuwai katika eneo hilo kama udhibiti wa dhati usipo chukuliwa kwa haraka kuinusuru eneo hilo la Delta ya Rufiji kaskazini.
Mradi huo wa hifadhi ya taifa ya Delta ya Rufiji kaskazini unafadhiliwa na Mfuko wa kundi la nchi maskini zaidi duniani (LDCF) kupitia Shirika la umoja wa Mataifa ya Mazingira chini ya usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment