Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja wa Wamiliki wa
kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam
ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya
viroba. Ofisi ya Makamu wa Raisi inaongoza uendeshaji wa ukaguzi wa
viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha na kutengeneza pombe
kali(viroba) na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.
Mwanasheria wa Baraza la
Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha waandishi wa
habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba) inayozalishwa na kampuni
hiyo pasipo kufuata kanuni za TFDA wala pasipo kuweka stika za TRA.
Mrundikano wa maboksi uliopo
kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za aina
mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuuza.
Mashine zinazotumiwa na kiwanda
cha Afro African Company kuzalisha pombe kali aina ya viroba pamoja na
kutengenezea vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe hizo
No comments:
Post a Comment