Wakili wa serikali Mkoani
Geita,Emily Kiria akielezea namna ambavyo jamii ya wanasheria
wanavyoweza kutoa haki na usawa kwa uhalisia na kwa wakati usika.
Baadhi ya mawakili wa serikali na wananchi wakiwa wanasikiliza na kufatilia kilichokuwa kikiendelea. |
Wananchi wakisikiliza na kufatilia tukio lilivyokuwa likiendelea.
Wakili kutoka chama cha mawakili
Tanzania(Tanganyika law society),Bernad Otieno.akieleza namna ambavyo
mahakama inatakiwa kutoa haki kwa wananchi.
Kaimu hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa
Geita,Kariho Mrisho,,akiendelea kutoa maelezo namna mahakama
ilivyojipanga kuendelea kutoa haki.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,Meja jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga,akisisitiza swala la maadili kwa watumishi wa mahakama
Mkoani Humo.
Lothan Simkoko akitoa neno la shukrani kwa watu ambao wamejitokeza kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya mawakili wakiwa kwenye picha ya pamoja.
……………………………………………………………….
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Jamii ya wanasheria
Mkoani Geita imetakiwa kutoa haki kwa misingi na sheria ikiwa ni pamoja
na kuzingatia swala la muda kwenye kesi ambazo wanazisimamia.
Kauli hiyo imesemwa na wakili wa
serikali Mkoani humo Emily Kiria wakati wa maadhimisho ya wiki ya
sheria,ambapo ameeleza kuwa jamii ya wanasheria wote wawe wa serikali
na wakujitegemea wanajukumu la kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na
ukweli kwa swala usika.
“Jamii ya wanasheria na hili ni
jukumu la wanasheria wote wawe wa serikali au wa kujitegemea wanalo
jukumu la kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na kwa ukweli wa swala
usika na siyo kuhakikisha tu kwamba wanawatetea au kuwasaidia watu
kwasababu tu wamefika kuomba msaada”alisema Kiria
Kwa upande wake wakili kutoka
chama cha mawakili Tanzania(Tanganyika law society),Bernad
Otieno,alifafanua kuwa mahakama inawajibu wa kusikiliza malalamiko
yanayoletwa na wananchi na kuyatolea mahamuzi wajibu huo ni wa kikatiba
kwani inatokana na jamhuri ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho
katiba ibara ya 107 (A) ibara ndogo ya kwanza na ya pili.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,Meja jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga ,ameendelea kusisitiza swala la muda wa kusikiliza kesi
,pamoja na kuwataka watumishi wa mahakama kuwa wahadilifu na waaminifu
kwenye shughuli zao.
“Naomba kutoa wito kwa watumishi
kuendesha kesi kwa muda usika ikiwa ni pamoja na kuwa waaminifu katika
shughuli zenu za kila siku za kutoa haki kwa wananchi”alisisitiza Kyunga
Siku ya Sheria nchini
ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na
Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi ambapo kitaifa imefanyikia jijini
Dar es salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli,kauli mbiu ikiwa ni Utoaji haki kwa
wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
No comments:
Post a Comment