Rais wa chama cha walimu Tanzania ( CWT ),Gracian Mkoba akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mvomero mhe. Mwl Mohammed Utali kuzindua vitabu vya kiingereza vilivyoandikwa na walimu wa Tanzania walio pata mafunzo ya uandishi wa vitabu (kulia), Mkurugenzi mtendaji wa Pana African Teacher’s center kutoka Ghana mwl Peter Mabande
Hafla ya uzinduzi huo ulifanyi kati ofisi ya chama hicho zilizopo kinondoni jijini Dar es Salaam -jumatatu Februari 27, 2017
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mvomero mhe. Mwl Mohammed Utali akisoma hotuba yake wakati akizundua vitabu vya kiingereza vilivyoandikwa na walimu wa Tanzania walio pata mafunzo ya uandishi wa vitabu.
Mkurugenzi mtendaji wa Pana African Teacher’s center kutoka Ghana mwl Peter Mabande akielezea kuhusina na kusaidia watoto wa Africa katika kujifunza lugha ya kiingereza wakati wa uzinduzi huo.
Walimu wakishuhudia uzinduzi huo wa vitabu.
Mgeni rasmi Mkuu
wa wilaya ya Mvomero mhe. Mwl Mohammed Utali (katikati) pamoja na
walimu wa chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
uzinduzi huo wa vitabu. (Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog ) …………………………………. |
Chama
cha walimu Tanzania ( CWT) kwa kushirikiana na shirikisho la Vyama
vya walimu Duniani kupitia OFISI ya Afrika kitengo cha kuendeleza
walimu kitaaluma (ILAF) Leo kimezindua vitabu vya kiingereza
vilivyoandikwa na walimu wa Tanzania walio pata mafunzo ya uandishi wa
vitabu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa vitabuhivyo Rais wa chama cha walimu Tanzania
Gracian Mkoba amesema vitabu hivyo vya hadith za kubuni vitasaidia
wanafunzi washule za msingi na sekondari katika kujifunza lugha ya
kiingereza , na vita gawanywa kwa majaribio katika wilaya ya mvomero
vikipata mafanikio vitasambazwa nchi nzima.
Amesema
katika mafunzo hayo walimu 36 wamefadika na mafunzo huku walimu watano
wakitika Zanzibar na walimu 31 wame toka Tanzania bara, na vitabu
vilivyo ingizwa katika mpango huo ni vya walimu 17 kati ya walimu 36
walio hudhuria mafunzo hayo ambavyo vilionekana kukidhi vigezo.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Mvomero mhe. Mwl Mohammed Utali ameshukuru chama
cha walimu kuiteua wilayahiyo katika mradi huo ,na kusema kuwa vitabu
hivyo vitasaidia kwa kuwa maeneo mengi ya wilaya hiyo ni ya familia za
wafugaji wanao hamahama hivyo kupewa vitabu hivyo kutawasaidia kuinua
kiwango cha Elimu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Pana African Teacher’s center
kutoka Ghana mwl Peter Mabande amesema wanameanzisha mpango huo
kimataifa ili kusaidia watoto wa Africa katika kujifunza lugha ya
kiingereza kutoka na hapo awali walimu hawakulipa umuhimu Mkubwa suala
la utunzi wa vitabu , na amekipongeza cha cha walimu Tanzania kuitikia
mpangohuo na kuupaumuhimuna has a kukubalikughalimia vitabu hivyo na wao
wataendelea kusaidia katika kutoa mafunzo kwa walimu.
No comments:
Post a Comment