CHANZO BBC
Mawasiliano
ya simu kati ya Rais wa Marekania Donald Trump na waziri mkuu wa
Australia Malcolm Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya
kuwachukua wakimbizi.
Gazeti la Washington Post
liliripoti kuwa bwana Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi
kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo
aliikata simu hiyo.
Bwana Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.
Makubaliano hayo yaliyoafikiwa
wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta hifadhi
1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini Marekani.
Australia imekataa kuwakubali
wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na Iraq
na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya
Nauru na Papua New Guinea.
Waziri mkuu Turnbull amekuwa
akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya
kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi
kuingia nchini Marekani.
Bwana Turnbull baadaye alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.
Alikiambia kituo kimoja cha redio mjini Sydney kuwa ripoti kwamba Trump alikata simu si za ukweli
No comments:
Post a Comment