Wakili wa
kujitegemea Mruma aShabibu kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku
hii ni maalum kwa mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila
malipo yeyote.
………………………………………
Na Pamela Mollel,Arusha
Imeelezwa
kuwa siku ya sheria ni siku ambayo wananchi wanapata fursa ya kupata
msaada wa kisheria ambayo kila mwananchi anapaswa kuwa chini ya shieria
na sio juu ya sheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake wakili wa kujitegemea Mruma
aShabibu kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku hii ni maalum kwa
mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.
Alisema
kuwa kwa siku hii watu wengi ufaidika kwa kutatuliwa baadhi ya matatizo
yao bila kutozwa gharama yeyote ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya
kisheria sanjari na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na mawakili.
Alidai
kuwa wananchi wanapaswa kuheshimu katiba lakini pia na kukaa chini ya
sheria ili haki iweze kutendekea kwani baadhi ya wananchi wanakaa juu ya
sheria hali ambayo inawafanya kujiona hawatendewi haki.
Hata
hivyo alifafanua kuwa lengo la kuanzishwa kwa siku hii ni kuangalia
umuhimu wa sheria katika jamii na kuona jinsi inavyofanya kazi katika
kukuza uchumi wa nchi
No comments:
Post a Comment