Pages

Thursday, February 2, 2017

SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA UJENZI WA BARABARA ZINAZOPITISHA MAGARI MACHACHE


UZI
Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng.  Ven Ndyamukama, akitoa hotuba ya utangulizi katika uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa  na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
UZI 1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
UZI 2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akikata utepe kwenye kitabu cha Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mara baada ya kuuzindua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa AFCAP Kanda ya Mashariki na Kati mwa Afrika, Eng. Nkulule Kaleta.
UZI 3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akimkabidhi nakala ya kitabu cha Mwongozo wa Ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mmoja wa wadau waliohudhuria uzinduzi huo, leo jijini Dar es Salaam.
UZI 4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (wa nne kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe  waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache hapa nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
………………..
Serikali imezindua mwongozo wa mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache kwa lengo la kutoa maelekezo na kuwawezesha wahandisi wanaofanya usanifu wa barabara hizo kutumia gharama nafuu za ujenzi.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema kuwa mwongozo huu utakuwa tiba na kuwezesha Serikali kujenga barabara nyingi na gharama nafuu.
“Ujenzi na ukarabati ya barabara zinazopitisha magari chini ya 300 kwa siku utakuwa wa gharama nafuu, kama tutatumia mwongozo huu kwani utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili barabara nyingi hususan za vijijini”, amesema Katibu Mkuu.
Amewataka wahandisi na Mafundi ujenzi kutumia mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.
“Hakikisheni wahandisi na Mafundi ujenzi mnafuata mwongozo huu ipasavyo na kuanzia sasa uwe dira kwenu katika kazi zenu za kila siku”,  amesisitiza Eng. Nyamhanga.
Ameongeza kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa Serikali imegundua uhitaji mkubwa katika mtandao wa barabara nchini ili kusaidia maendeleo ya kila mwananchi mijini na vijijini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara hiyo Eng. Ven Ndyamukama amesema kuwa mwongozo huo  unafananua namna ujenzi wa barabara hizo unavyokuwa ikiwemo kujenga kulingana na idadi ya magari yanayopita.
Ameongeza kuwa Mwongozo huo unaelekeza kutumia rasilimali chache zilizopo na kuhakikisha masuala ya mazingira  katika maeneo yanayojengwa barabara hizo yatazingatiwa.




No comments:

Post a Comment