Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Mratibu Elimu Kata (MEK) ni mmoja
kati ya kiungo kikubwa kati ya ofisi ya elimu ya wilaya na shule za
serikali katika ngazi ya kata ambaye ndiye mfuatiliaji mkubwa wa
maendeleo ya
elimu ndani ya kata.
Shughuli nyingine zinazofanywa na
MEK ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya taalamu ya wanafunzi katika
kata yake, kukagua ufundishaji wa walimu, kufuatilia mahudhurio ya
wanafunzi pamoja na kusimamia vikao mbalimbali vya shule zilizoko katika
kata yake.
Asilimia kubwa ya Waratibu Elimu
Kata walikuwa wanashindwa kufikia malengo ya kazi zao kutokana na
changamoto ya usafiri, ambapo wengi wao walikuwa wakitumia usafiri wa
baiskeli ambao ha
ukuwa
usafiri rafiki kutokana na kazi yao ya kukagua shule zote katika kata
wanazozisimamia.
Serikali kwa kuliona hilo,
kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (Education Quality
Improvement Programme -Tanzania) EQUIP-T ilitoa pikipiki kwa kila MEK
katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Shinyanga, Simiyu na Mara ili
kurahisha ufuatiliaji wa mendeleo ya shule zao kwa urahisi.
Pikipiki hizo zimeleta mafanikio
makubwa kama vile kupungua kwa idadi ya wanafunzi watoro, kiwango cha
ufaulu kupanda kutokana na ukaguzi wa mara kwa mara wa walimu pamoja na
matatizo kutatuliwa kwa haraka kutokana na taarifa za shule kufika
wilayani kwa wakati.
Sweetbert Malimi ni Mratibu Elimu
Kata wa Sanzawa Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma anasema kwamba Pikipiki
imemuwezesha kushughulikia kwa wakati matatizo yanayotokea katika shule
anazozisimamia tofauti na kipindi ambacho hakuwa na pikipiki.
Anaendelea kwa kusema kuwa,
matatizo yalipokuwa yakitokea katika shule anazosimamia yalikuwa
yakimsubiri MEK hata kwa mwezi mzima. Lakini sasa hivi imekuwa tofauti
kutokana na kutembelea shule zake hata mara mbili kwa wiki.
Vilevile ameweza kufuatilia kwa
wakati maendeleo ya taaluma ya wanafunzi pamoja na ufundishaji wa walimu
ambapo kabla ya kuwa na pikipiki kuna baadhi ya walimu walijisahau
kutokana na kutokaguliwa mara kwa mara.
Anaendelea kwa kusema kuwa,
ufuatiliaji huo umeletea mafanikio makubwa katika Mkoa wa Dodoma, ambapo
ufaulu wa darasa la saba kwa wilaya ya Chemba peke yake ulipanda kutoka
asilimia 30 mwaka 2015 mpaka asilimia 46 mwaka 2016.
Kwa upande wake Mratibu Elimu
Kata wa Songambele iliyoko Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma amesema kuwa
katika kata yake ana shule Sita za kuzifuatilia ambapo kabla ya kupata
pikipiki alikuwa anatumia baiskeli kutembelea shule hizo na aliweza
kutembelea shule hizo mara moja kwa wiki.
Baada ya kupata pikipiki anauwezo
wa kutembelea shule hizo mara tatu hadi nne kwa wiki akifuatilia
maandalio ya walimu, maazimio ya kazi, utengenezaji wa zana za
kufundishia, mahudhurio ya wanafunzi pamoja na kuhudhuria vikao vya
kamati ya shule.
Aidha amesema kuwa, kutokana na
ufuatiliaji huo wa mara kwa mara katika shule hizo kumepelekea umakini
mkubwa wa ufundishaji wa walimu kwa kufuata taratibu za ufundishaji kama
vile kuwa na maandalio, maazimio ya kazi pamoja na kuwa na zana za
ufundishaji.
Pia amesema kwamba kwa kutumia
pikipiki aliyopewa amekuwa akiwatembelea wazazi ambao watoto wao ni
watoro, na kuwashauri juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wao na wazazi
wenyewe. Juhudi hizo zimepelekea wazazi wengi kubadilika na kushirikiana
na walimu katika kufuatilia mahudhurio na maendeleo ya taaluma ya
watoto wao.
Nae, Mratibu Elimu Kata wa Kagera
wilaya ya Kigoma Manispaa, Mkoa wa Kigoma Jovitus Augustus anasema
kuwa kabla ya kupewa pikipiki kata yake ilikuwa na changamoto ya utoro
kwa wanafunzi pamoja na ufaulu duni wa wanafunzi wa darasa la saba.
“Pikipiki niliyopewa kupitia
mpango w EQUIP-T umeniwezesha kutengeneza mipango kazi ya wiki na
kuisambaza katika shule zote za kata pamoja na kufuatilia utekelezaji
wake,” alifafanua Jovitus.
Aliendelea kwa kusema kuwa
pikipiki hiyo imemuwezesha kukagua utekelezaji na utoaji taaluma kwa
kukagua maazimio ya kazi na maandilio ya somo pamoja na kufanya vikao
vya mara mara kwa mara na walimu ili kupata maelezo ya walimu
walioshindwa kutekeleza wajibu wao.
Aidha kupitia juhudi hizo
zilizofanyika, ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba shule za msingi za
kagera na Mgumile ulipanda pmoja na mahudhurio ya walimu na wanafunzi
katika kata hiyo umeongezeka .
Vilevile umeanzishwa utaratibu wa
mitihani ya kata kwa darasa la saba pamoja na kuweka kambi kwa
wanafunzi wanaojiandaa na mitihani wa darasa la Saba.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa
Shule ya Msingi ya Mazoezi Bunda iliko Halmashauri ya Mji Bunda Mkoa wa
Mara, Mwalimu Vicent Ndunguru, aliipongeza Serikali kupitia Mpango wa
EQUIP-T kwa kutoa pikipiki kwa Waratibu Elimu Kata ambao kwa kiasi
kikubwa umewarahisishia utendaji kazi wao.
Amesema kuwa, kulikuwa na mambo
mengi ambayo yalikuwa hayaendi inavyotakiwa kutokana na MEK anayosimamia
shule yake kutotembea shule hiyo mara kwa mara kutokana na ukosefu wa
usafiri wa uhakika.
Amesema kuwa, baada ya MEK huyo
kupatiwa pikipiki amekuwa akitembelea shuleni hapo mara kwa mara
kufuatilia maendeleo ya shule na kuchukua taarifa za shule na
kuziwasilisha wilayani kwa wakati.
Mwalimu Ndunguru ambaye pia ni
msaidizi wa MEK katika kata ya Nyasura amesema kuwa, MEK huyo amekuwa
akiitisha vikao vya mara kwa mara kujadili maendeleo ya shule katika
kata yake. Ambapo Shule ya Msingi Mazoezi Bunda ndio eneo lilochaguliwa
kwa ajili ya kufanyia mikutano hiyo.
Aliendelea kwa kusema kuwa, MEK
huyo amekuwa chachu ya maendeleo ya shule zilizoko katika kata hiyo hasa
baada ya kuwa na uhakika na usafiri ambao kwa asilimia kubwa
umemuwezesha kufanya kazi zake kwa urahisi na hata kufikia malengo
aliyowekewa na mwajiri wake na yale aliyojiwekea yeye mwenyewe katika
kuhakikisha ubora wa elimu uaongezeka siku hadi siku kutoka ngazi ya
kata mpaka Taifa.
Aidha Mwalimu Ndunguru, ameiomba
Serikali kuendeleza na utaratibu wa ugawaji wa pikipiki kwa Waratibu
Elimu Kata wa mikoa mingine iliyobaki ili na wao waweze kufanya kazi kwa
ufanisi kama ambavyo wenzao waliopewa pikipiki ambavyo wameweza
kufanikiwa na hata kupandisha kiwango cha ufaulu na kukomesha tatizo la
utoro kwa wanafunzi.
Serikali kupitia mpango huo pia
umetoa vishikwambi kwa Waratibu Elimu Kata hao, ambao wamekuwa wakitumia
vifaa hivyo kwa ajili ya kupokea taarifa kutoka kwa walimu wakuu wa
shule wanazozisimamia na wao kuzituma taarifa hizo ofisi za elimu za
wilaya.
Mpango wa EQUIP-T umetoa jumla ya
pikipiki 1,000 kwa Waratibu Elimu Kata wa mikoa ya Dodoma, Kigoma,
Lindi, Shinyanga, Simiyu, Shinyanga na Mara. Pikipiki hizo zilitolewa
kati ya mwaka 2014 na 2015 ambapo mpango huo unawawezesha waratibu hao
kupata fedha ya mafuta na utengenezaji wa pikipiki hizo kila mwezi
No comments:
Post a Comment