Na Judith Mhina –MAELEZO
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
yafaulisha wanafunzi 743 kati ya watahiniwa 784 na kushika nafasi ya
Tatu Kitaifa kati ya Halmashauri 178hapaTanzania.
Katika mahojiano maalum na Idara
ya Habari MAELEZO Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Kakonko Bw Lusubilo Joel
Mwakabibi amesema: “Shule za serikali zimeanza kurudisha heshima ya
kufaulu kama ilivyokuwa miaka ya 1970 na 1980, mara baada ya matokeo ya
kidato cha Nne mapema mwezi huu”.
Mwakabibi ameeleza kuwa
Halmashauri hiyo inajumla ya shule za sekondari 14, kati ya
hizo 11 ni za Serikali na 3 za binafsi. Matokeo ya kidato cha nne
mwaka huu
Yanaonesha daraja la kwanza
shule za binafsi ni 10, pili 35, tatu 40, nne 41 na zilizopata ziro ni
13. Kwa upande wa Shule za Serikali daraja la kwanza 6, pili 47, tatu
149, nne 400 na ziro 38.
“Siri ya mafanikio yetu ni
usimamizi wa karibu na ufuatiliaji shuleni, umoja na mshikamano kati ya
Walimu, wazazi, Viongozi wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa wilaya;
walimu wetu tupo pamoja nao, tunawatia moyo katika kazi ya kufundisha”.
Anafafanua Mkurugenzi huyo.
Aidha, Mkurugenzi Mwakabibi
amesema mwaka 2016 Halmashauri imeshika na fasiyatatu, Kitaifa katika
Halmashauri 178 Tanzania, kwani matokeo ya kidato cha Nne na Pili mwaka
2015, Halmashauri yetu, ilikuwa ya kwanza kitaifa na kuzawadiwa ngao ya
ushindi toka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. Hata hivyo ameeleza
kuwa mikakati ya Halmashauri yake ni kurudi namba moja, lengo likiwa ni
kuhakikisha wanafunzi wote watakao sajiliwa kufanya mtihani wa kufaulu
kwa viwango vya juu na kufuta kabisa aibu ya kufeli..
Bw Mwakabibi amesema kati ya
watahiniwa 794 wa Kidato cha Nne 743 wamefaulu na wanafunzi 51 tu ndio
waliofeli. Shule ambayo imeongoza matokeo ya kidato cha nne ni ya
binafsi ya Mtakatifu Thomas More Kibogora iliyotahini wanafunzi 30,
mbili za binafsi matokeo yake ya kosa wana shule zetu za serikali na
idadi ya wanafunzi ni 55. Huu niuthibitisho dhahiri kuwa shule za
Sekondari za Serikali zenye watahiniwa 709 ambazo ni Kata zimefanya
vizuri kama shule za binafsi.
Kuhusu masomo waliyofaulu,
Mwakabibi amesema kuwa watahiniwa wamefanya vizuri zaidi katika masomo
ya Uraia (Civics), Historia, Biolojia, Kingereza, Jiografia, na
Kiswahili na kubainisha kuwa ufaulu ni matokeo ya uwepo wa walimu
wakutosha na wenye uwezo mkubwa wa ufundishaji na kufanya kazi kwa bidii
na kujituma
“Ili tuendelee kuwa namba moja,
Halmashauri inasimamia walimu katika kazi zao, inawahudumia na kujali
mahitaji yao. Pia, inashirikiana na shule, wazazi, wadau wengine
iliwanafunzi wajifunze kwa bidii na vitendo iliwapate maarifa na kutumia
elimu yao katika maisha ya kila siku, vilevile halmashauri ipate
matokeo bora zaidi”. Amesema Mwakabibi
Mwakabibi alisisitiza kuwa
“Mafanikio yetu ya mechangiwa na wazazi, walimu, Ofisi ya Mkurugenzi,
Waheshimiwa Madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na wadau mbalimbali kama
Mpango wa Ubora wa Elimu Tanzania EQUIP-T , kwa kuunda Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (Parent Teachers Participation).
“Ushirikiano huu, umesaidia
kuwatia hamasa wazazi kushirikiana vizuri na walimu katika zoezi zima la
kuchangia chakula, kwa kutoa mahindi kilo tano kila mzazi kwa muhula
mmoja”. Alifafanua Mkurugnezi huyo na kuongeza kuwa hatua hiyo
imewezesha watoto kuwa na usikivu wakati wa ufundishaji na ujifunzaji
na kuongeza ufaulu”.
Akichangia utoaji wa chakula
shuleni Afisa Elimu Sekondari Bw Joseph Mutahaba amesema “Kakonko
imefanikiwa kutoa chakula au uji katika shule za Msingi 59 zaserikali”.
Huu ni utekelezaji wa agizo la Serikali la wanafunzi kupata chakula
wawapo shuleni. Zoezi hili limefanikiwa baada ya kuhamasisha na
kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa kuchangia chakula au uji kupitia
vikao mbalimbali.
Bwana
Mutahab Alitoa Wito kwa
Halmashaurinyinginekuhakikishakuwazianakuwana:“Usimamiziwakaribuwataalumashuleni,
kuwajali walimu, kuwapa moyo, kuwasikiliza shida zao, kuwahamasisha
wafundishe kwa bidii, ushirikiano wa karibu wa wazazi, walimu na wadau
wengine wa Elimu katika kuboresha mazingira ya ujifunzaji na
ufundishaji” na kusisitiza kuwa “Haya ni mambo ya msingi sana”.
Tofauti na Halmashauri nyingine
ambazo zina shule nyingi za binafsi ambazo hunyanyua viwango vya ufaulu
wa Halmashauri hizo lakini kwa upande wa Kakonko ambayo ina idadi ndogo
ya shule za binafsi, shule za Serikali zimesaidia kunyanyua kiwango cha
ufaulu hadi kushika nafasi ya tatu Kitaifa katika Halmashauri.
Ulinganisho huo umefanywa kwa kupata maelezo ya:
Afisa Elimu Mkoa wa Njombe Bw
Halfan Omary Masukira amesema: “Halmashauri ya Mji Njombe shule za
binafsi zilizotahiniwa 16; daraja la kwanza 58, pili167,tatu 162, nne
168 naziro 12. Shule zaserikalizipo15 daraja la kwanza 11, pili
61,tatu146,nne584 naziro 105 jumlawatahiniwa 1538”
Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa
Kagera Bw Wandare Lwakatare amesema: Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
shule za binafsi zilizotahiniwa 13; daraja la kwanza 133, pili 209, tatu
171, nne 188 na ziro 16. Kwa upande wa Shule za serikali ni 16; daraja
la kwanza 24, pili 97, tatu 167, nne 550 na ziro 190 jumla watahiniwa
1757.
Ukiangalia takwimu za Halmashauri
hizo tatu utagundua kuwa shule za Kata za Kakonko zimefanya vizuri
kuliko za Kata za Halmashauri ya kwanza na ya pili. Halmashauri ya
kwanza Tanzania katika ufaulu wakidato cha nne ni Manispaa ya Bukoba;
kati yawatahiniwa 1757 waliofaulu ni 1542, waliofeli 215 na kupata GPA
ya 3. 5414 ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe ambayo ilikuwa na
watahiniwa 1538 na walifaulu 1418, waliofeli 120 na kupata GPA 3.6453.
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ndio iliyoshika nafasi ya tatu ambayo
ilikuwa na watahiniwa 794 kati yao watahiniwa waliofaulu ni 743 na
waliofeli ni 51 na kupata GPA ya 3.6716. Kakonko ndio Halmashauri yenye
wanafunzi watahiniwa wachache zaidi katika Halmashauri kumi bora.
No comments:
Post a Comment