Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa
Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam
kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango
wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri
nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni
Mstaafu John Chiligati.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi
wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA)
Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao
baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa
mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene,
Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
Mratibu wa MKURABITA Bibi.
Seraphia Mgembe akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya
Uongozi ya MKURABITA na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa
mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati na
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo
Lupala.
Watendaji kutoka Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Miji Dkt. Mkuki Hante pamoja na Mkurugenzi wa Utawala kwa
Serikali za Mitaa Bibi. Miriam Mmbaga wakifuatilia mjadala wakati wa
kikao baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na MKURABITA
kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akipokea taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango
wa Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52
na Miji 9 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita
Kapteni Mstaafu John Chiligati leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akisoma taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa
Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na
Miji 9 nchini mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati(hayupo pichani) leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa
Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati (katikati) Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala mara baada ya
mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya hiyo Ofisini kwake leo Jijini
Dar es Salaam.
Na: Mpiga Picha Wetu.
……………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija – MAELEZO.
27/02/2017
Kufuatia kusuasua kwa utekelezaji
na maendeleo ya Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara
Serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini ambazo zimefikia na mpango
huo
kuwasilisha taarifa rasmi.
Agizo hilo limetolewa na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George
Boniphace Simbachawene katika kikao baina yake na wajumbe wa Kamati ya
Uongozi wa MKURABITA kilichofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar es
Salaam.
Simbachawene amesema kuwa
TAMISEMI ni mdau muhimu katika Mpango huo wa urasimishaji wa rasilimali
hivyo ujio wa kamati hiyo kutaka kushirikiana na Tawala za Mikoa ni
jambo jema.
“Binafsi ni muumini wa muda mrefu
wa mpango huu wa urasimishaji, niseme tu mmechelewa kuja sehemu husika
kwa bila dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi kufanikiwa kwa
mpango huu itakuwa ni adithi sasa tutaenda pamoja ili kiutimiza azma ya
mpango huu,”alisema Simbachawene.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Kapteni wa Jeshi Mstaafu John Chiligati
amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa Halmashauri zaidi ya 100 nchini mpaka
sasa utekelezaji wa mpango huo umezifikia takribani Halmashauri 52 na
Miji 9 tu hivyo kasi yake bado hairidhishi.
Aliongeza kuwa changamoto
wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa mpango huo ni Halmashauri
kuuona mpango huo kama hawahusiki nao hali inayopelekea kushindwa
kuendelea pindi mwakilishi wa Mkurabita atakapo ondoka katika eneo
husika.
Chiligati amesema kuwa baada ya
kubaini changamoto hiyo waliamua kuwa na makubaliano maalum na TAMISEMI
juu ya utekelezaji wa pamoja wa mpango huo jambo ambalo wanaendelea
kulifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment