Pages

Monday, February 27, 2017

Afya Kwanza ya TBL Group yatawala mashindano ya Kilimanjaro Marathon


afya1
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari kushiriki mbio za Kili Marathon
afya2
Taswira ya furaha kwa wafanyakazi wa TBL Mwanza wakati wanapanda  gari kuelekea Moshi kushiriki Kili marathon 2017
afya3
Taswira ya furaha kwa wafanyakazi wa TBL Mwanza wakati wanapanda  gari kuelekea Moshi kushiriki Kili marathon 2017
………………………………………………………………………………
-Wafanyakazi  wake washiriki kwa wingi
 
Mpango wa wafanyakazi kufanya mazoezi na kupima afya zao unaotekelezwa na kampuni ya TBL Group ujulikanao kama Afya Kwanza  umeonekana kuwa na manufaa makubwa katika kujenga afya ambapo umewezesha idadi kubwa ya wafanyakazi wake kutoka mikoa mbalimbali kushiriki katika mashindano ya riadha ya Kili Marathon yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 
Baadhi ya wafanyakazi wakizungumzia ushiriki wao walisema kuwa wanajivunia kuwa na mpango huo wa kujenga afya ambapo umewawezesha  kushiriki vizuri na kumalizia mbio zao bila kujali umri wa mtu.
 
Pia waliishukuru kampuni yao kwa kufanikisha mipango ya wafanyakazi wake wote kutoka mikoa mbalimbali kuwa na wawakilishi wa kushiriki mashindano hayo ambayo mdhamini wake mkuu ni TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro.
Meneja wa Programu hiyo,Julieth Mgani,alisema kuwa tangia programu hiyo ianze mwaka jana imeonyesha kuwa na mafanikio makubwa na wafanyakazi wengi wameikubali kwa kushiriki kufanya mazoezi mara kwa mara,Kuzingatia matumizi sahihi ya vyakula na kupima afya zao  kwao binafsi na familia zao.
 
“Moja ya mafanikio ni wafanyakazi wengi wa kampuni kushiriki mashindano haya bila wasiwasi wowote kutokana na kufanya mazoezi mara kwa mara,na tunaendelea kuimarisha program hii zaidi na kuyashirikisha makundi mbalimbali kwenye jamii kwa kuwa suala la mazoezi kwa ajili ya kujenga afya linamhusu kila mtu”.Alisema.

No comments:

Post a Comment