Picha na Chris Mfinanga
Mke wa Marehemu Kapteni Kenan Mhaiki akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake.
Watoto wa Marehemu Kapteni Kenan Muahiki wakiweka Mashada ya maua katika kaburi la Baba yao.
Waziri
mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za serikali katika misa ya
kumuombea marehemu Kapteni Kenan Mhaiki iliyofanyika katika kanisa la
Jimbo kuu Katoliki la Songea Parokia ya Mtoto Yesu Matogoro Songea.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameongoza mamia ya wakazi wa mji wa Songea na kata ya Matogoro kuuaga
mwili wa aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali
(TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki katika ibada iliyofanyika kwenye parokia
ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu iliyoko Matogoro, mjini Songea.
Waziri Mkuu ambaye ameshiriki
msiba huo kwa niaba ya Serikali, pia alishiriki mazishi ya Kapteni
Mhaiki ambaye pia alikuwa rubani wa ndege za Serikali yaliyofanyika
kwenye makaburi ya parokia ya Matogoro.
Akizungumza kwenye ibada ya
mazishi mara baada ya kutoa heshima za mwisho, leo jioni (Jumatano,
Januari 4, 2017), Waziri Mkuu aliwasilisha salamu za rambirambi kutoka
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
“Msiba huu ni wetu sote na
umetugusa wote. Ni msiba mzito kwa wanafamilia na kwa Serikali pia.
Kapteni Mhaiki amekuwa rubani wa ndege za Serikali kwa muda mrefu na
amewaendesha viongozi wa kitaifa kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya
tano. Kwa niaba ya Serikali tunawapa pole sana,” amesema.
“Ninawaomba wafiwa wote hasa mke
wa marehemu na watoto tushikamane katika kipindi hiki na tuendelee kuwa
wavumilivu huku tukimuombea Baba yetu apate pumziko la milele,” amesema.
Kapteni Mhaiki alifariki dunia
Desemba 31, 2016 katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam.
Alilazwa katika hospitali hiyo, kabla ya sikukuu ya Krismasi, kwa
ugonjwa wa saratani ya ini.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 4, 2017.
No comments:
Post a Comment