Pages

Sunday, January 29, 2017

TBL Group yang’ara tuzo za Tanzania Leadership Awards 2016


TIB1
Afisa Mawasiliano  wa TBL Group Amanda  Walter (Kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Meneja mkuu wa kituo cha televisheni cha TV 1,Joseph Sayi ,  wakati wa hafla ya tuzo kwa makampuni na taasisi zilizofanya vizuri katika nyanja mbalimbali  ya    Tanzania Leadership Awards 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro    jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
TIB2
Balozi wa Moroco nchini, Abdelilah Bennjane,  (kushoto) akimkabidhi  Meneja wa  Chapa ya Ndovu  ,Nicholous John (kulia)  tuzo ya ushindi  wa jumla  kwa kipengele cha Mitandao ya kijamii ( Social Media Campaign of the year)  TBL ilishinda  kipengele hicho kupitia kampeni yake ya Mwagika Challenge Tanzania.
TIB3
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, Mohammed  Mpinga, (kushoto) akibadilishana mawazo na   Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda  Walter (katikati) na Meneja wa  Chapa ya Ndovu ,Nicholous John  wakati wa hafla ya Tanzania Leadership Awards iliyofanyika  jijini mwishoni mwa wiki.Jeshi la polisi lilitunukiwa tuzo ya ubunifu wa huduma mbalimbali katika utendaji wake wa kazi -Most  Innovative Service of the  Year 2016  
TIB4
Afisa Mawasiliano  wa TBL Group Amanda  Walter na Meneja wa  Chapa ya Ndovu  ,Nicholous John wakiwa na tuzo ambazo TBL imejishindia
……………………………………………………..
Kampuni ya TBL Group mwishoni mwa wiki iliendelea na rekodi yake ya kufanya vizuri katika Nyanja mbalimbali ambapo ilifanikiwa kuzoa tuzo kuhusiana na masoko na matangazo katika hafla ya Tanzania Leadership Awards iliyofanyika  jijini mwishoni mwa wiki.
TBL iliwepata tuzo kupitia chapa ya Ndovu Special Malt ambayo ilipata tuzo ya jumla katika kipengele cha Print Ad of the Year na tuzo ya jumla katika kipengele cha matangazo kupitia mitandao ya kijamii kupitia kampeni yake ya Mwagika Challenge Tanzania.
Akiongelea ushindi huo,Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter ,alisema kuwa kampuni inajivunia ushindi huo wa tuzo hizo “Tuzo hizi zinadhihirisha kuwa kampuni yetu inafanya vizuri katika nyanja mbalimbali ambapo taasisi mbalimbali zinaona ubora wa kazi zetu na kutupatia tuzo ,kwetu tuzo hizi zinazidi kutufanya wabunifu zaidi na tutaendelea kuboresha huduma zetu na kushirkiana na serikali na taasisi zizizo za kiserikali kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuleta maendeleo kwa nchi yetu”.Alisema.

No comments:

Post a Comment