Diwani wa viti maalum,Kibaha Mjini
Selina Wilson akimwombea kura mgombea mteule kupitia CCM kata ya
Misugusugu katika uzinduzi wa uchaguzi mdogo katika kata hiyo.
Katibu wa CCM mkoani Pwani,Hassan Mtenga akizungumza jambo katika kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Misugusugu
Mgombea mteule kupitia CCM kata ya Misugusugu,Ramadhani Bogas akiomba kura kwa wakazi wa Misugusugu katika uzinduzi wa kampeni .
Baadhi ya wana CCM na wakazi wa
Misugusugu wakicheza katika uzinduzi wa kampeni kata ya
Misugusugu,uchaguzi katika kata hiyo unarejea baada ya kutenguliwa na
mahakama ya mkoa wa Pwani.
Katibu wa CCM mkoa wa Kusini
Unguja ,Sauda Mpambalioto ,akimuombea kura mgombea mteule wa ugombea
udiwani kupitia CCM ,Kata ya Misugusugu Ramadhani Bogas.(Picha na
Mwamvua Mwinyi).
……………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
KATIBU wa chama cha mapinduzi
(CCM)mkoani Pwani,Hassan Mtenga,amevitaka vyama pinzani viache
kudanganya watanzania kuwa hakuna maendeleo yanayofanywa na serikali na
badala yake vifanye tathmini na kwenda na data ili kupata majibu.
Aidha amesema mwenye macho aambiwi tazama ,ni ukweli unaoonekana
kuwa serikali ya awamu ya tano kupitia CCM inatekeleza ilani yake kwa
kuleta maendeleo ya wananchi.
Akizungumza katika uzinduzi wa CCM
katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Misugusugu ,Mtenga alisema
wakazi wa kata hiyo wasikubali kudanganyika wakati wanaiona serikali
inavyochapa kazi.
Mtenga alieleza kuwa
,wapinzani kwa sasa wamezimwa,hawana jipya ,wanatapatapa hivyo
watanzania wawapuuze kwa mambo ya uzushi wanayoyaibua.
Alisema kuna kila sababu ya
kuwajibu wachache wanaojaribu kuiharibia sifa serikali kwa yale
inayoyafanya ili kuwakomesha wasiendelee kuipaka matope.
“WanaCCM tafuteni kura kwa umoja
wenu,msijiamini kwa kutafuta kura majukwaani,kura hazipatikani kwenye
majukwaa pekee ,fanyeni kazi,tumieni maarifa ,piteni nyumba kwa nyumba
kupata kuipa ushindi CCM”alisema Mtenga.
Katibu huyo wa CCM mkoani
hapo,akijibu hoja zinazoibuliwa kwenye kampeni zinazofanywa na Chadema
katika kata hiyo, alieleza kwamba ,hali ya kiuchumi wa Tanzania
unaelekea kwenye asilimia 9 kutoka nne.
Aliwataka wasiropoke kwenye
majukwaa pasipokuwa na tatwimu halisi,waache kuongea bila kuwa na data
hali inayosababisha kupotosha watanzania.
Kuhusu miundombinu alifafanua
kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma ni km 641 ambapo watanzania
wanatembea kwenye lami,Mtwara hadi Dar es salaam km 514,Dar es
salaam-Iringa km 500.1 ni lami ,Dodoma –Mwanza km 334.Mwanza -Geita
kupitia Nyakanazi yenye km 644 nayo ni lami.
Mtenga alisema Tanzania lazima
ijivunie kuwa na miundombinu ya barabara bora kwa kiwango cha lami
ambapo kwasasa inafikia km 18,900.
Nae katibu wa CCM mkoa wa Kusini
Unguja ,Sauda Mpambalioto ,alimuombea kura mgombea mteule wa ugombea
udiwani kupitia CCM ,Ramadhani Bogas na kusema anafaa kuwa kiongozi na
sio bora kiongozi.
Alisema upinzani haumaanishi hata
penye sifa kukatolewa dosari na badala yake kwenye sifa ama maendeleo
haina budi pakaungwa mkono.
Sauda alisema CCM imefanya mengi ndani ya nchi tofauti na miaka 50 iliyopita hivyo ambae haoni maendeleo hayo ana lake jambo.
Mjumbe wa halmashauri Kuu ya
CCM Taifa Kibaha Mjini, Rugemalira Rutatina, aliwaasa vijana kuacha
kutumika kama ngazi na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.
Rutatina ,alisema sio wakati wa
kuchanganya madalanzi na machungwa hivyo wakazi hao wachague diwani wa
CCM ili kupiga hatua kimaendeleo.
Kwa upande wake ,mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala alisema anaimani na Bogas kwani ni mtu makini na muwajibikaji.
Aliwaomba wakazi wa Misugusugu kumchagua Bogas ili kutimiza majifya matatu ikiwa ni pamoja na rais,mbunge na diwani.
Mgombea udiwani kupitia CCM katika kata hiyo,Bogas aliwaomba
wakazi wa kata hiyo kumpa kura ili kushirikiana kuinua maendeleo yao.
Aliahidi kutatua kero mbalimbali zinazogusa sekta ya elimu,afya,miundombinu kwa kuzifikisha sehemu husika na kupatiwa ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment