Na Mahmoud Ahmad Arusha
JUMLA
ya kaya 704 mkoani Arusha ambazo hazina sifa zimeondolewa kwenye mpango
wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa kupitia TASAf ,a kuagiza
uhakiki zaidi ufanywe ili kubaini kaya zilizoingizwa kwenye mpango huo
zikiwa hazina sifa ziondolewe mara moja.
,
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ,Richard Kwitega,ameyasema hayo Desemba 27
mjini Loliondo, wilayani Ngorongoro, kwenye kikao cha kutathimini
utekelezaji wa TASAF awamu ya tatu pamoja na Programu ya OPEC awamu ya
tatu ambapo mipango yote hiyo inalenga kuzisaidia kaya masikini
kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza
kwenye kikao hicho cha kazi chawatendaji wote wa TASAF mkoani Arusha,
Katibu tawala huyo ameagiza watendaji wote waliohusikakuingiza kaya zisizo
na sifa kwenye mpango huo wachukuliwe hatua za kinidhamu ikiwemo
kurejesha fedha hizo ili zitumike kusaidia sehumu nyingine
Amesema
jumla ya kaya 44643 ziliandikishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na
zilistahili kupata Malipo ya kwanza mwezi Julai na Augosti mwaka 2015 ambapo zilipokelewa jumla ya shilingi 1,854, 369,500 .
Amesema mpaka sasa mkoa umepokea awamu tisa za malipo ya ruzuku kwa kaya masikini ambapo shilingi 17,159,438,634 zimeshapokelewa na kati ya hizo shilingi 15328653294 zimehaulishwa kama ruzuku kwa walengwa huku shilingi 1,830, 785 339 zimetumika kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za mpango huo.
Kwitega, amesema mwezi Mei mwaka 2016 serikali ilipokea ujumbe wa benki ya dunia na kufanya nao mazungumzo juu ya makundi yanayoishi kwenye mazingira magumu ikiwa ni kuangalia utekelezaji wa mpango wa kunusuru makundi maalumu.
Ameongeza kuwa ujumbe huo umetembelera wilaya ya Karatu,mkoani Arusha ili kuona,kuzungumza na walengwa ili kuonas makabila yanayoishi kwenye mazingira magumu wilayani humo yanaandikishwa kwenye mpango huo wa kunusuru kaya masikini.
Tayari kaya 2080 zimeandikishwa wilayani Karatu katika tarafa ya Eyasi kuanzia Augosti 2016
Kwitega,
amesema pamoja na mafanikio ya TASAF awamu ya tatu bado yapo maeneo
ambayo wananchi wanahitaji kusaidiwa katika kujikwamua na umaskini
uliokisiri.
Kwa upande Kaimu Mkurugenzi wa TASAF Omari Malilo, amezitaka halmashauri za wilaya kukamilisha miradi hiyo kabla ya mwezi Februari, 2017.
Programu hiyo inaendeshwa ndani mpango wa kunusuru kaya makini (TASAF,111ambayo vijiji na mitaa iliyopo kwenye mpango huo ilizinduliwa rasmi kitaifa mkoani Arusha, mei 3 mwaka 2015 ambapo nchini program hiyo inatekelezwa kwenye mikoa miwili ya Arusha na Njombe kwa ufadhili wan chi zinazozalisha na kuuza mafute Ulimwenguni OPEC,
Ambapo wananchi wamekuwa wakiibua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu, Elimu, Afya .
Ambapo
mkoa wa Arusha katika kutekeleza mpango ghuo umeibua jumla ya miradi 63
na tayari shilingi 1,556, 709, 896 zimetolewa kupitia TASAF na miradi 43 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake ambapo jumla ya shilingi 2,748, 468, 978,zimetengwa ili kukamilisha miradi yote 63
No comments:
Post a Comment